Hori
Hori ni sehemu ya mwambao wa bahari au ziwa inayozungukwa na nchi kavu pande tatu. Ni kidogo kuliko ghuba, mara nyingi husababishwa na mdomo mto kwenye bahari na kuelekea ndani ya bara.
Hori mara nyingi ni mahali pazuri kwa ajili ya bandari asilia kwa sababu imelindwa kisi na nguvu ya mawimbi.