Bandari asilia ni mahali panapofaa kama kituo cha meli kutokana na tabia zake za kiasili. Nafasi ya aina hii inapatikana mara nyingi katika kidaka, kwenye hori au mdomoni wa mto penye kinga dhidi ya upepo na hasa mawimbi ya bahari. Tabia nyingine inayohitajika ni kina cha maji kinacholingana na mahitaji ya meli zinazotumia bandari.

Vidaka vinafaa kama bandari asilia
Bandari ya Dar es Salaam kwenye mdomo pana wa mto Kurasini unaoingia barani kwa kilomita kadhaa

Sharti hili la kina lamaanisha ya kwamba bandari asilia inaweza kuonekana haitoshi tena kwa mahitaji ya meli zilizokuwa kubwa zaidi.

Mifano ya mabandari asilia

hariri
  • Dar es Salaam: bandari iko katika hori kubwa ambalo ni mdomo pana wa kijito kidogo lenye urefu wa kilomita moja katika beseni ya kwanza na kilomita 3 katika beseni ya kusini. Meli zinaingia kutoka bahari kupitia mlango mwembamba wa 270 m pekee hivyo imelindwa kabisa na mawimbi. Bandari hii asilia ilikuwa sababu ya kuhamishwa kwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kutoka Bagamoyo.
  • Mombasa ina bandari asilia nzuri ya Kilindini ambacho ni pia hori inayoingia ndani. Kisiwa cha Mombasa kipo katika mdomo wa hori baharini. Bandari ya Kilindini ina urefu wa kilomita tano na upana wa kilomita tatu imezungukwa na nchi kavu poande zote hivyo imelindwa kabisa.

Bandari asilia kubwa nyingine duniani ni:

Kilwa Kisiwani ni mfano wa bandari asilia nzuri ambayo haitumiki tena kwa sababu kina cha maji hakitoshi kwa meli za kisasa.