Hospitali ya Lugalo
Hospitali ya Lugalo ni hospitali inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ikiwa ndani ya Kambi ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Ilianzishwa mwaka 1955 kwa ajili ya jeshi la kikoloni la Kiingereza King's African Rifles katika eneo la kambi la kijeshi Dar es Salaam iliyoitwa wakati ule Colito Barracks. Kwa wakati huo ikijulikana kama kituo cha mapokezi (Medical Reception Station) ikiwa na uwezo wa kulaza wagonjwa thelathini.[1]
Baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 hospitali hii ilianza kutoa huduma kwa wanajeshi wa Tanganyika Rifles, tangu 1964 kwa jeshi jipya la Tanzania na ikiwalenga wanafamilia wa wanajeshi hao waliokuwa wakiishi jirani na kambi hiyo ya jeshi.
Wakati wa Vita vya Kagera hospitali hii ilijukana kama "Lugalo Garrison Hospital" ikitumika kama kituo cha madaktari wa dharura kwa wapiganaji waliokuwa wakihudumu katika uwanja wa vita.
Marejeo
hariri- ↑ Afya Ilihifadhiwa 6 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |