Hukwe Zawose (Bugiri, 1940 - Bagamoyo, 30 Desemba 2003) alikuwa mwanamuziki wa kiasili wa kitanzania, na muziki wake hasa ulikuwa wa kabila la Wagogo. Ala aliyotumia zaidi ilikuwa ilimbal pamoja na zeze; alipiga pia filimbi.

Hukwe Zawose mnamo mwaka 2003 kwenye Jubilee Diamnond Hall, Dar es Salaam(picha:Issa Michuzi)
Wanawe Hukwe Zawose wanaendeleza muziki yake (picha:Issa Michuzi)

Kipaji chake cha muziki kiligunduliwa na aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania hayati J. K. Nyerere wakati alipofanya ziara mkoa wa Dodoma. Alivutiwa na muziki wa Hukwe, na aliporudi Dar es Salaam alimuita Hukwe kwenye kikundi cha utamaduni cha Taifa Bagamoyo Players.

Katika miaka ya 1990 Zawose alirekodi muziki pamoja na Peter Gabriel na kutoa CD kadhaa.

Albamu Kadhaa hariri

Viungo vya Nje hariri

Sikiliza hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hukwe Zawose kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.