Hydrox
Hydrox ni aina ya kuki iliyojazwa chokoleti ambayo ilianzishwa katika mwaka wa 1908 na ikatayarishwa na Kampuni ya Sunshine Biscuits. Jina lake la Hydrox linatokana na vipengele vya atomu vinavyounda maji: hasa haidrojeni na oksijeni. Baadhi ya ripoti kadhaa ,inasemekana kuwa Oreo ,iliyoanzishwa baadaye katika mwaka wa 1912, ilikuwa imeundwa ikiiga mfano wa Hydrox. Ingawaje, Hydrox imeshambuliwa na wengi kuwa bidhaa hii ilikuwa ikiiga Oreo. Ikilinganishwa na Oreo, kuki ya Hydrox ilikuwa inaonja "tamu kidogo" na ilikuwa ngumu na bora kuliwa na maziwa.
Uzalishaji
haririSunshine Biscuits ilinunuliwa na kampuni ya Keebler katika mwaka wa 1996 na katika mwaka wa 1999 ,Keebler ilibadilisha Hydrox na kuki zinazofanana na hizo mpya zilizoitwa Droxies. Keebler ilinunuliwa , baadaye, na kampuni ya Kellog's katika mwaka wa 2001. Kellog's ilitoa bidhaa za aina ya Droxies kutoka kwenye soko katika mwaka wa 2003. Kellog's ,hivi sasa, inauza kuki za chokoleti chini ya jina la Famous Amos. Mashabiki kadhaa wa Hydrox ya hapo awali hushuku kuwa hizi ni ni kuki za Hydrox zinazoanzishwa tena huku wengine wakitafuta furaha kwa kuki zingine kama za Newman-O's na zingine mbalimbali. Kampuni ya Kellog's husema upishi wa Hydrox ni wa kipekee usiojulikana na kampuni zingine.
Katika mwaka wa mia wa kuki hizi, Kellog's ilianzisha tena usambazaji wa Hydrox chini ya jina la Sunshine. Bidhaa za kwanza zilianza kusambazwa katika mwisho wa mwezi wa Agosti 2008. Mashabiki wa Hydrox waliisumbua kampuni ya Kellog's huku maelfu wakipiga simu na kuandika ombi la kutaka kuki hizo zitayarishwe tena. Upishi wa Hydrox mpya ulibadilishwa kidogo kutoka ile ya zamani; walitoa mafuta ya aina ya trans-fats kutoka matumizi katika upishi. Kuki hizo zilikuwa zinafaa kupatikana katika taifa zima kwa muda mfupi lakini baada ya muda chini wa mwaka mmoja Kellog's ilitoa Hydrox kutoka tovuti yao.
Kampuni ya Carvel ya kuunda vyakula vya aina ya ice cream huuza ice cream zilizotayarishwa na makombo ya kuki za "Hydrox". Carvel inatumia hali ya kuki hizo ya all-kosher kama mbinu ya kuongeza mauzo kama vile Oreo ya hapo awali ilitumia mafuta ya nguruwe. Kuki hizi hazitajwi kwa jina katika tovuti ya Carvel lakini katika mabango yake yaliyowekwa ndani ya maduka kuki hizo zimeandikwa kama kuki za hydrox (jina likiwa na "h" ndogo).
Marejeo
hariri- Paul Lukas (15 Machi 1999). "Oreos to Hydrox: Resistance Is Futile". Fortune.
- Christopher Rhoads (19 Januari 2008). "The Hydrox Cookie Is Dead, and Fans Won't Get Over It". The Wall Street Journal.
- Christopher Rhoads (28 Mei 2008). "Hydrox Redux: Cookie Duels Oreo, Again". The Wall Street Journal.
- Carvel
Viungo vya nje
hariri- Ukurasa wa Hydrox Cookie Ilihifadhiwa 25 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Hydrox Redux: Cookie Duels Oreo, Again
- Carvel