I'll Be There

"I'll Be There" ni wimbo uliotungwa na Berry Gordy, Bob West, Hal Davis na Willie Hutch ambapo baadae ulikuja kutokea nyimbo mbili , yaani wimbo ambao ulikuja kurekodiwa na kundi la nchini Marekani la The Jackson 5 . Mwaka 1992 na wimbo huu uliimbwa na mwanamziki wa Marekani Mariah Carey katika onesho la moja kwa moja pamoja na mwanamuziki mwingine ambaye pia ni wa nchini Marekani Trey Lorenz.

“I'll Be There”
“I'll Be There” cover
Single ya The Jackson 5
kutoka katika albamu ya Third Album
B-side "One More Chance"
Imetolewa Agosti 28, 1970 (1970-08-28)
Muundo 7" 45 RPM
Imerekodiwa Hitsville West, Los Angeles in 1970
Aina Pop, soul, bubblegum pop
Urefu 3:57
Studio Motown
M 1171
Mtayarishaji Berry Gordy, Bob West, Hal Davis, Willie Hutch
Mwenendo wa single za The Jackson 5
"The Love You Save"
(1970)
"I'll Be There"
(1970)

Wimbo wa kundi la The Jackson 5, ulirekodiwa katika studio za Motown Records na kutolewa rasmi kama single ya kwanza katika albamu ya kundi hili, iliyoitwa Third Album . Hii ikiwa ni mwaka 1970. Ukiwa umetengenezwa na watunzi maahiri, wimbo wa I'll Be There ilikuwa wimbo wa tano wa kundi hili kufika katika nafasi ya kwanza mfululizo ukifuatia nyimbo za "I Want You Back," "ABC," na "The Love You Save." Wimbo wa "I'll Be There" umesemekana kuwa ndio wimbo wenye mafanikio zaidi kuwahi kutengenezwa katika studio za Motown katika kipindi chake cha Detroit ambacho ni kuanzia mwaka 1959-1972. Pia ni wimbo wa nne kutoka kwa kundi hili kufika katika nafasi ya kwanza mfululizo na hivyo kulifanya kundi hili kuwa kundi la kwanza la wavulana wenye asili ya Afrika kuwahi kufika katika nafasi hiyo.

Mwanamuziki mwingine wa Marekani Mariah Carey na Trey Lorez pia waliurudiwa wimbo huu katika kipindi cha MTV Unplugged mwaka 1992, na kuutoa katika albamu yake ya EP MTV, katika nusu ya tatu ya mwaka 1992. Wimbo huupia ulirekodiwa na Mwariah Carey kwa kushirikiana na Walter Afanasieff na wimbo huu ukawa wimbo wa sita Kutoka kwa Mariah Kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya single ya Marekani na pia ulikuwa wimbo uliofanya vizuri katika maeneo mbambali duniani.

Toleo la The Jackson 5Edit

Kuhusu rekodi hiiEdit

Baada ya nyimbo tatu kutoka kwa kundi la The Jackson ambazo ziliwahi kufika katika nafasi ya kwanza ni ("I Want You Back," "ABC," na "The Love You Save"). Mtunzi wa nyimbo Berry Gordy ndipo akaamua kutunga mashairi kwa ajili ya kundi hili. Alifanya hivi kwa kuwashirikisha watunzi mbalimbali kama vile Hal Davis, Willie Hutch, na Bob West, hii ikiwa ni tofauti na watunzi walioshiriki katika kutunga nyimbo tatu za kwanza.

Kutolewa na mapekeoEdit

Katika maandishi yake, Michael Jackson ansema kuwa wimbo wa I'll Be There umesaidia katika kurudisha umoja miongoni mwa The Jackson 5 kuwarudisha pamoja kuuthiitishia umma kuwa, kundi hili bado lina uwezo na nguvu wa kutoa nyimbo nzuri.".[1].

Wimbo huu ulifanya vizuri katika nafasi mbalimbali na kufanikiwa kuuza nakala zaidi milioni 4.2 nchini Marekani na nakala milioni 6.1 duniani pote, kuchukua nafasi ya nyimbo za Marvin Gaye "I Heard It Through the Grapevine" zilizopata mafanikio ikiwa ni pamoja na kushina nafasi za juu katika chati za muziki nchini Marekani. Nafasi hii ilichukuliwa na wimbo ulitolewa na wimbo kutoka kwa Lionel Richie akishirikiana na Diana Ross katika wimbo wa Endless Love wa mwaka 1981. Nji ya nchi ya Marekani wimbo uliobakia maarufu kutoka studio za Motown ni wimbo wa "I Heard It Through the Grapevine" kwa kufanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni 7 dunia nzima.

Wimbo huu ulishika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard Hot 100 kwa muda wa wiki 5, kuanzia tarehe 17 Oktoba hadi 14 Novemba, na kuchukua nafasi ya wimbo wa Cracklin Rosie ulioimbwa na Neil Diamond, na kiuchukua nafasi ya I Think I Love You ulioimbwa na Partidge Family. Wimbo wa "I'll Be There" pia ulikuwa wimbo bora na kushika nafasi ya kwanza katika chati ya R&B singles chart kwa muda wa wiki sita,[2] na kushika nafasi ya nne katika chati muziki ya nchini Uingereza.

ChatiEdit

Chati (1970) Ilipata
nafasi
Dutch Singles Chart[3] 18
Australian Singles Chart[4] 34
UK Singles Chart[5] 4
U.S. Billboard Hot 100 1
U.S. Billboard Black Singles 1
U.S. Billboard Easy Listening 24
Chart (2009) Kilele
UK Singles Chart 65[6]

Toleo la Mariah CareyEdit

“I'll Be There”
 
Single ya Mariah Carey featuring Trey Lorenz
kutoka katika albamu ya MTV Unplugged
Imetolewa Mei 26, 1992 (1992-05-26)
Muundo CD single, cassette single, 7" single
Imerekodiwa Kaufman Astoria Studios on 16 Machi 1992
Aina Pop, R&B
Urefu 4:25/4:42
Studio Columbia
Mtayarishaji Mariah Carey, Walter Afanasieff
Certification Gold (New Zealand)
Mwenendo wa single za Mariah Carey featuring Trey Lorenz
"Make It Happen"
(1992)
"I'll Be There"
(1992)
"If It's Over"
(1992)

Mariah Carey pia alijumisha wimbo hu katika onesho la MTV Unpluged na kuwa wimbo wa sita hii ikiwa ni tarehe 16 Machi 1992. Wimbo huu pia uliimbwa na Mariah Kwa kushirikiana na Michael Jackson pamoja na Trey Lorenz. na kuimba katika mashari aliyoimba Jarmaine Jackson.

"I'll Be There" ulichaguliwa katika moja ya nyimbo zilizokuwa katika kushindania tuzo yaGrammy Award for Best R&B Performance by a Duo or Group with Vocals, kwa mwaka 1993. Katika kumbukumbu ya Michael Jackson , tarehe 7Julai 2009, Carey na Lorez waliimba wimbo huu kama kumbukumbu ya Michael Jackoson

Orodha ya nyimboEdit

Worldwide CD single

 1. "I'll Be There"
 2. "So Blessed"

European CD maxi-single

 1. "I'll Be There"
 2. "So Blessed"
 3. "Vanishing"

UK CD maxi-single

 1. "I'll Be There"
 2. "Vision of Love" (live)
 3. "If It's Over
 4. "All in Your Mind"

Chart performanceEdit

Wimbo huu, umekuwa katika nafasi ya kwanza katika chati ya nyimbo 100 bora kuanzia terehe 13 Juni mwaka 1992 hadi tarehe 27. Hii ikiwa ni mara ya pili kwa wimbo huu kufika katika nafasi ya kwanza, na kuchukua nafasi ya wimbo wa "Jump" ulioimbwa na Kris Kross, a baadae nafasi hii ilichukuliwa na wimbo wa Baby Got Bacj ulioimbwa na Sir Mix-a-Lot . Wimbo huu uliongoza katika nyimbo zilizokuwa na mafanikio zaidi nchini Marekani katika chati ya Hot Adult Contemporary Tracks. Hata hivyo wimbo huu unabakia kuwa wimbo pekee, uliotolewa nastudio za MTV Unplugged na kufika gadi nafasi ya kwanza. I'll Be There ulikuwa wimbo wa kwanza kutoka kwa Caey kufanya vizuri nje ya Marekani ya Kasazini, na kuwa wimbo wenye mafanikio katika masoko mbalimbali. Uliweza kushika nafasi ya kwanza katika chati ya single ya Canada kwa kipindi cha wiki mbili, na kuwa wimbo wake wa kwanza kuwahi kufanya vizuri katika soko la Uingereza ambapo ilishika nafasi ya 2, na nchini Australia ulishika nafasi ya 9.

Ulishika nafasi mbalimbali katika nyimbo ishirini bora katika soko la Ulaya ambapo Mariah Carey hakuweza kufanya hivyo hapo kabla.

Washiriki
Toleo Data Watayarishaji
The Jackson 5 Berry Gordy
Bob West
Hal Davis
Willie Hutch
Mariah Carey Mariah Carey
Walter Afanasieff

ChatiEdit

Chati (1992) Ilipata
nafasi
Australian Singles Chart[7] 9
Canadian Singles Chart[8] 1
Dutch Singles Chart[9] 1
French Singles Chart[10] 16
German Singles Chart[11] 33
Irish Singles Chart[12] 3
New Zealand Singles Chart[13] 1
Norwegian Singles Chart[14] 10
Swedish Singles Chart[15] 26
Swiss Singles Chart[16] 20
UK Singles Chart[17] 2
U.S. Billboard Hot 100[18] 1
U.S. Billboard Hot Adult Contemporary Tracks[18] 1
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs[18] 11

MauzoEdit

Provider Sales Certification
New Zealand 7,500+ Gold
United States 1,000,000+ Platinum

Wengine waliourudiaEdit

Kundi la The Temptations waliurudia wimbo huu katika albamu yao ya Reflections. Halikadhalika kundi la Westlife waliurudia wimbo huu katika albamu yenye jina lao wenyewe. New Kids on the Block covered the song live on the day of Jackson's death.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

 1. allmusic.com[dead link]
 2. Whitburn, Joel (2004). Top R&B/Hip-Hop Singles: 1942-2004. Record Research, 287. 
 3. Dutch Singles Chart
 4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-03-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-23.
 5. UK Singles Chart
 6. UK Singles Chart. The Official UK Charts Company. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2009.
 7. Australian Singles Chart
 8. Canadian Singles Chart
 9. Dutch Singles Chart
 10. French Singles Chart
 11. German Singles Chart
 12. Irish Singles Chart
 13. New Zealand Singles Chart. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-06-21. Iliwekwa mnamo 2010-01-23.
 14. Norwegian Singles Chart
 15. Swedish Singles Chart
 16. Swiss Singles Chart
 17. UK Singles Chart
 18. 18.0 18.1 18.2 Artist Chart History - Mariah Carey. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-04-04. Iliwekwa mnamo 2008-04-04.