Jadakiss
Jason Phillips (amezaliwa tar. 27 Mei 1975),[1] anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jadakiss, ni rapa kutoka nchini Marekani. Huyu ni mwanachama wa kundi zima la The LOX. Jadakiss ni mmoja kati ya wamiliki wa chapa ijulikanayo kama D-Block.
Jadakiss | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Amezaliwa | 27 Mei 1975 Yonkers, New York, U.S. |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapper |
Miaka ya kazi | 1993–hadi leo |
Studio | D-Block, Ruff Ryders, Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | The LOX, Styles P, Sheek Louch, DMX, Swizz Beatz, Raekwon, Jay-Z, Fat Joe, Rick Ross, Pharrell |
Maisha binafsi
haririAkiwa na umri wa 16, Jadakiss alikuwa rapa wa michano huru. Yeye na baadhi ya marafiki zake walipewa fursa ya kushiriki kwenye shindano la "Jack the Rapper Competition" huko mjini Florida, ambapo Jadakiss aligunduliwa kipaji chake cha kupambana kirap. Akakutana na Dee na Wah wa Ruff Ryders (halafu kuongoza kampuni), na kuanza kazi kuzura kimapambano ya michano nje ya studio ya Ruff Ryders ambapo baadhi ya wasanii kama vile DMX wamefanya vibao vyao kwa mara ya kwanza.
Kazi
haririJadakiss ameanzisha kundi la The Warlocks kunako mwaka wa 1994 akiwa na washkaji zake Sheek Louch, Chris "Lil Mac" Pelkey, na Styles P. Baadaye wakaingia mkataba na Bad Boy Entertainment, ambapo walishauriwa kubadili jina lao liwe fupi kuwa "The LOX", ambayo inasimama kama Living Off eXperience. Wameanza kuonekana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa kwenye LP ya The Main Source mnamo 1994 Fuck What You Think katika wimbo wa "Set it Off".
Kundi, hasa Jadakiss, amejenga uhusiano wa karibu sana na The Notorious B.I.G., kipindi hicho Jadakiss yupo begani mwa Biggie. Kibao cha kwanza cha The LOX kilitolewa kama ukumbusho wa Biggie kiliitwa "We'll Always Love Big Poppa" (upande wa pili wa wimbo wa Puff Daddy "I'll Be Missing You") mnamo 1997.Mwaka wa 1998, kina LOX wametoa kibao cha Money, Power & Respect. Baada ya albamu hii, wameondoka Bad Boy Records.
Diskografia
hariri- Studio albums
- 2001: Kiss tha Game Goodbye
- 2004: Kiss of Death
- 2009: The Last Kiss
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Smith, Kerry L. (2004). "Jadakiss > Biography". allmusic. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2008.
Viungo vya Nje
hariri- Official website
- Jadakiss katika MySpace
- Jaheim ft. Jadakiss- Every time I think About Her Official Music Video Ilihifadhiwa 4 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- Jadakiss at his Coogi Photo Shoot Ilihifadhiwa 4 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- Backstage with Jadakiss at the Highline Ballroom Ilihifadhiwa 4 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- Photos from Jadakiss' set at SXSW 2009 from Phrequency.com Ilihifadhiwa 11 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- Jadakiss interview with HHC Digital magazine Ilihifadhiwa 15 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- Jadakiss top 5 dead or alive Ilihifadhiwa 9 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.