Jahazi
Jahazi (Kiarabu جهاز chombo) ni mashua yenye tanga ambayo hutumika kubeba watu na shehena (mizigo).
Leo hutumika katika kazi za uvuvi kwa wavuvi wadogowadogo na matumizi ya usafiri, pia kama chombo cha burudani au mashindano ya kukimbizana.
Kabla ya matumizi ya injini za mvuke na injini za diseli kwenye meli kulikuwa na jahazi kubwa zilizotekeleza usafiri wa baharini. Jahazi kubwa za mwisho ziliacha kutumiwa kibiashara kwenye miaka ya 1950.
.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |