Uvuvi ni kazi ya kukamata samaki ndani ya maji na kuwaweka nje yake, lakini pia kufuga samaki na wanyama wengine wa majini.

Wavuvi katika bandari ya Kochi, India.

Kusudi lake ni hasa kupata chakula (kitoweo) na watu wengine hufanywa kama biashara kujipatia kipato. Siku hizi pia watu hushiriki uvuvi kama burudani, katika utalii na kama sehemu ya michezo.

Uvuvi ni kati ya shughuli za kale kabisa za binadamu na katika uchumi wa nchi nyingi huhesabiwa kati ya sekta msingi pamoja na kilimo na uchimbaji wa madini. Kutokana na takwimu za FAO kuna watu milioni 38 duniani wanaofanya kazi ya kuvua au kufuga samaki na hivyo husaidia kukuza uchumi wa nchi fulani. Pamoja na wanaosafirisha windo wanaofanya kazi viwandani, na wanao uza masokoni, madukani na hotelini kuna zaidi ya watu milioni 500 wanaokimu maisha yao kutokana na sekta hii ya uvuvi. [1]

Uvuvi hufanywa penye magimba ya maji kama vile bahari, maziwa, mito au mabwawa. Mara nyingi wavuvi hutumia chombo cha kusafiria majini kama boti lakini wengine wanakaa ufukoni na kuvua kutoka nchi kavu.

Vyombo vya uvuvi ni aina za nyavu zinazoweza kushika samaki na kumvuta nje ya maji, ndoano au pia aina za mikuki inayolenga samaki walio karibu na uso wa maji.

Tunapaswa kulinda bahari, maziwa pamoja na mito ili mazalia ya samaki yazidi kuongezeka na pia tupige vita uvuvi haramu kwa kuwa husababisha kuwa nyuma kwa sekta ya uvuvi.

Inabidi serikali ziweke ulinzi kwenye suala la uvuvi kwani kuna wavuvi haramu wanaotumia sumu, baruti na vinginevyo vingi ambavyo havitakiwi katika uvuvi.

Marejeo hariri

  1. ftp://ftp.fao.org/FI/brochure/climate_change/policy_brief.pdf[dead link] Fish (including shellfish) provides essential nutrition for 3 billion people and at least 50% of animal protein and minerals to 400 million people in the poorest countries. • Over 500 million people in developing countries depend, directly or indirectly, on fisheries and aquaculture for their livelihoods. • Aquaculture is the world’s fastest growing food production system, growing at 7% annually. • Fish products are among the most widely traded foods, with more than 37% by volume of world production traded internationally.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uvuvi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.