Jaji Mkuu wa Zanzibar
Jaji Mkuu wa Zanzibar ni jaji mkuu wa Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yeye huteuliwa na Rais wa Zanzibar kwa kushauriana na Tume ya huduma za kimahakama na ndiye anayeongoza Mahakama Kuu ya Zanzibar.[1]
Historia
haririZanzibar ilikuwa nchi iliyolindwa na Uingereza kufuatia Makubaliano ya Anglo-German ya mwaka 1890.
Amri ya Baraza iliunda Mahakama Tukufu ya Kibritania kwa ajili ya Zanzibar ikiwa na jaji kiongozi mwaka 1897.
Amri nyingine ilianzisha Mahakama Kuu mwaka 1925.
Usultani wa Zanzibar ilipata uhuru wake mnamo Desemba 1963 na baada ya mapinduzi mwezi mmoja baadaye uligeuzwa kuwa Jamhuri ya Unguja na Pemba.
Mwaka 1964 iliunganishwa na Tanganyika na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambayo baadaye mwaka huo ilibadilishwa jina na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya kuunganishwa sehemu zote mbili za jimbo jipya zilihifadhi mifumo yao ya zamani ya mahakama.
Majaji wakuu Zanzibar
hariri- 1897–1901: Walter Borthwick Cracknall
- 1901–1904: George Bettesworth Piggott
- 1904–1914: Lindsey Smith
- 1915–1919: James William Murison
- 1919–1925: Thomas Symonds Tomlinson
Majaji wakuu Zanzibar
hariri- 1925–1928: Thomas Symonds Tomlinson
- 1928–1933: George Hunter Pickering
- 1934–1939: Charles Ewan Law
- 1939–1941: John Verity
- 1941–1952: John Milner Gray
- 1952–1955: George Gilmour Robinson
- 1955–1959: Ralph Windham
- 1959–1964: Gerald MacMahon Mahon
- 1964–1969: Revolutionary Council (Chief Justice: Geoffrey Jonas Horsfall)
- 1970–1978: Ali Haji Pandu
- 1985–2011: Hamid Mahmoud Hamid
- 2011–2021: Omar Makungu[2]
- 2021- Khamis Ramadhan Abdalla
Tazama zaidi
haririMarejeo
hariri- ↑ "Zanzibar: Constitution". Electoral Institute of Southern Africa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Juni 2012. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lubuva New NEC Chairman". www.tmcnet.com.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |