Jalidi ni hali ya baridi ambapo halijoto inafikia chini ya kiwango cha sentigredi 0. Hii ni kiwango ambako maji yanaanza kuganda kuwa barafu.

Jalidi husababisha kuganda kwa mvuke wa maji uliopo hewani ukikusanyika kwenye matawi ya miti

Jalidi kama halijoto inaathiri viumbehai na mimea kwa sababu huwa na maji katika miili yao. Mimea inakufa katika hali ya jalidi kama maji ndani ya seli zao inaganda; maji yakiganda yanapanua mjao wake hivyo kupasua seli. Mimea hiyo au sehemu zao zilizokufa huwa nyeusi na hali hii hutiwa jalidi pia (kwa Kiingereza: black frost).

Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa majira ya baridi ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika mazingira ya joto mimea hufa mara nyingi kama baridi huwa kali.

Kama hali ya jalidi inaendelea kwa wiki mfululizo inaathiri pia ardh,i yaani udongo. Ardhi yenyewe inaganda hadi kimo fulani kinachotegemea muda wa kudumu kwa jalidi. Kwa hiyo mabomba ya maji yanawekwa chini ya ardhi kwenye kimo ambako kwa kawaida jalidi haifiki. Hata hivyo, kama majirabaridi ni kali sana maji yanaweza kuganda ndani ya mabomba na kupasua bomba. Katika mazingira yenye jalidi kunatokea pia uharibifu wa barabara kama maji ya mvua yameingia katika tako la barabara au katika mapengo madogo kwenye lami na kuganda baadaye; maana maji yaliyoganda hupanuka kidogo na hivyo kupasua lami.

Katika mazingira baridi sana kama Aktiki au Antaktiki jalidi inaingia katika udongo hadi kimo cha mita kadhaa. Katika mazingira hayo majirajoto ni mafupi mno, hivyo kuna sehemu za juu za ardhi pekee zinazopoa lakini chini yake bado kuna jalidi ya kudumu (ing. permafrost). Hii inazuia uoto wa miti na kutokea kwa tundra kwa mfano katika maeneo mapana ya Urusi wa Kaskazini na Alaska.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jalidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.