Janvière Ndirahisha

Mwanasiasa na Msomi wa Burundi


Janvière Ndirahisha (kuzaliwa Burundi, 1966) ni msomi na mwanasiasa. Kutoka mwaka 2015 mpaka 2020 alikuwa waziri wa elimu nchini Burundi. Ni rais wa National Women's Forum (FNF).

Janvière Ndirahisha
Tarehe ya kuzaliwa 1966
Mahali pa kuzaliwa Burundi
Kazi Mwanasiasa

Maisha hariri

Janvière Ndirahisha aliyapata masomo yake kutoka Chuo Kikuu cha Burundi akaendelea kupata shahada ya uzamili kutoka University of Antwerp. Tasnifu yake kuhusu Grothiendiek representations ilisimamiwa na Fred Van Oystaeyen.[1]

Ndirahisha alichaguliwa kuwa Rais wa kongamano jipya la kimataifa la wanawake Burundi katika mwaka wa 2013.[2]

Katika mwaka wa 2015, Agosti, Ndirahisha alitangazwa kama Waziri wa Elimu, Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi katika baraza la mawaziri la Pierre Nkurunziza [3] Kufikia mwaka wa 2019 alikuwa ameshakuwa Waziri wa Elimu, Ufundi na Mafunzo ya Ufundi naye Gaspard Banyankimbona akiwa Waziri wa Elimu, Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi [4]

Katika mwaka wa 2017, Ndirahisha alitangaza kuwa walimu wakuu wa shule ambazo zilikuwa zimepata chini ya asilimia thelathini, 30% katika mitihani ya kitaifa wangeachishwa kazi na wizara yake ikafunga shule kadhaa zilizofeli. [5] Katika mwaka wa 2018 wizara yake ikapiga marufuku wasichana wajawazito kutoka kuhudhuria shule, hatua ambayo ilikosolewa na wapigania haki sawa nchini.[6]

Mrithi wa Rais Nkurunziza Évariste Ndayishimiye aliondoa Ndirahisha kutoka baraza la mawaziri mnamo mwaka wa 2020.

Marejeo hariri

  1. Scott W. Williams. "Janviere Ndirahisha". Black Women in Mathematics. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021. 
  2. Diane Uwimana (26 May 2014). "Women's forum: a slow step". IWACU English News. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.  Check date values in: |date= (help)
  3. "Government of Burundi". Embassy of the Republic of Burundi in Ankara. 24 August 2015. Iliwekwa mnamo 21 February 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "Burundi". The Economist Intelligence Unit. 1 May 2019. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2021.  Check date values in: |date= (help)
  5. Diane Uwimana. "Six "unauthorized" basic schools to be closed in Bujumbura". Iliwekwa mnamo 21 February 2021.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. Nita Bhalla. "Burundi school ban on expectant teens 'skewed' against girls' education", 4 July 2018. 
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Janvière Ndirahisha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.