Japhet Nyang'oro Sudi

Japhet Nyang'oro Sudi (amezaliwa Dar es Salaam, 18 Januari 1981) ni mwandishi wa riwaya za kipelelezi kutoka nchini Tanzania.

Japhet amejizolea umaarufu kwa uwezo wa kubuni riwaya za kipelelezi huku akimtumia mpelelezi wake mkuu katika riwaya zake nyingi, Jacob Matata.[1] Alitoa riwaya yake ya kwanza mnamo mwaka wa 2014 na ilikwenda kwa jina la Hekaheka.

Japhet Nyangoro Sudi ni mhitimu wa shahada ya uzamili wa sayansi za kifedha.

Vitabu alivyoandikaEdit

Hii ni orodha ya vitabu vilivyoandikwa na Japhet:

 1. Hekaheka - (2013)
 2. Ni Zamu yako Kufa - (2014)
 3. Mkono wa shetani- (2014)
 4. Patashika - (2015)
 5. Msako - (2016)
 6. Msako II - (2016)
 7. Saa 72 - (2017)
 8. Patapotea - (2018)
 9. Oparesheni Panama - (2018)
 10. Mdhamini- (2019)
 11. Love & leftovers - (2019)

MarejeoEdit

 1. Page. somariwaya.co.tz. Iliwekwa mnamo 2020-01-26.