Jengo la Bharmal, Zanzibar
Urithi wa Dunia katika Zanzibar
Jengo la Bharmal, Zanzibar liko katika mtaa wa Malindi ndani ya Mji Mkongwe[1].
Awali lilisimama pembezoni mwa kijito kilichogawanya Mji Mkongwe kutoka Ng'ambo. Leo jengo hilo linasimama pembezoni mwa barabara karibu na kijito, baada ya mkondo kurudishwa polepole kati ya miaka 1915 na 1960.
Historia
haririHapo awali lilijengwa kama makazi ya mfanyabiashara tajiri wa India, Mohamedbhai Sheikh Hoosenbhai, kisha likatumika kama ofisi za utawala wa Uingereza, na leo inatumika kama ofisi za Baraza la Manispaa la Zanzibar (ZMC).
Marejeo
hariri- ↑ Bharmal Building, tovuti ya archnet.org (taasisi ya Aga Khan)
Makala hii kuhusu majengo ya kihistoria Zanzibar bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jengo la Bharmal, Zanzibar kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |