Ofisi kwa ujumla ni chumba au eneo lingine ambalo kazi ya utawala hufanywa, lakini pia inaweza kuonyesha nafasi katika shirika na kazi maalum zinazohusiana nayo (tazama afisa, mmiliki wa ofisi) kutimiza wajibu wa mtu. Katika hali ya sasa ofisi kawaida inahusu sehemu ambako huajiri wafanyakazi wa kuvaa shati jeupe.

Ofisi ya kisasa ya kawaida.
Ofisi inayorahisisha ushirikiano huko London, Uingereza.
Ofisi ya hospitalini.

Ikiwa hutumiwa kama kivumbuzi, neno "ofisi" linaweza kutaja kazi zinazohusiana na biashara. Kama ilivyo kwa James Stephenson, "Ofisi ni sehemu ya biashara inayojitolea kwa uongozi na ushirikiano wa shughuli zake mbalimbali." Kisheria, kampuni au shirika lina ofisi mahali popote ambazo zina uwepo rasmi, hata ikiwa uwepo huo una, kwa mfano, ghala badala ya ofisi.

Ikiwa ni ofisi ndogo, kama vile benchi katika kona ya biashara ndogondogo ya kawaida, kupitia sakafu nzima ya majengo, mpaka ikiwa ni pamoja na majengo makubwa yaliyotolewa kabisa kwa kampuni moja.

Ofisi za kale zilikuwa sehemu ya jumba au hekalu kubwa. Miaka 1000-1300 iliona kuongezeka kwa mahali ambapo barua nyingi za serikali ziliandikwa na ambapo sheria zilikopiwa katika utawala wa ufalme.

Pamoja na ukuaji wa mashirika makubwa, katika karne ya 18, nafasi za kwanza za kujengwa kwa madhumuni zilijengwa. Mapinduzi ya Viwanda yalipostawi katika karne ya 18 na 19, viwanda vya benki, reli, bima, rejareja, mafuta ya petroli, na simu vilikua kwa kiasi kikubwa, na makarani wengi walihitajika. Kwa sababu hiyo ofisi zaidi zilihitajika kwa shughuli hizi na kuruhusu mameneja kuona kirahisi wafanyakazi.

Hata hivyo, katikati ya karne ya 20, ikawa dhahiri kuwa ofisi inayofaa ilihitaji busara katika udhibiti wa faragha, na hatua kwa hatua mfumo wa chumba ulibadilishwa.

Lengo kuu la mazingira ya ofisi ni kusaidia washiriki wake katika kufanya kazi yao. Kazi katika ofisi hutumiwa kwa shughuli za kawaida za ofisi kama vile kusoma, kuandika na kazi za kompyuta. Kuna aina tisa ya ofisi, kila moja kusaidia shughuli tofauti. Mbali na vyumba vya mtu binafsi, kuna vyumba vya mkutano, viungio, na nafasi za shughuli za msaada, kama vile kupiga picha na kusafirisha. Ofisi nyingine pia zina eneo la jikoni ambako wafanyakazi wanaweza kuandaa chakula cha mchana.

Kuna njia nyingi za kupanga nafasi katika ofisi nazo zinatofautiana kulingana na kazi, mitindo ya usimamizi na utamaduni wa kampuni maalumu yanaweza kuwa muhimu zaidi.

Wakati ofisi zinaweza kujengwa karibu na eneo lolote na karibu na jengo lolote, baadhi ya mahitaji ya kisasa ya ofisi hufanya iwe vigumu zaidi, kama vile mahitaji ya umeme, mitandao, na usalama.

Kusudi la msingi la jengo la ofisi ni kutoa mahali pa kazi na mazingira ya kazi hasa kwa wafanyakazi wa utawala na usimamizi. Mara nyingi wafanyakazi hao huchukua maeneo ya ndani ya jengo la ofisi, na kwa kawaida hutolewa na madawati, kompyuta na vifaa vingine vinavyohitajika ndani ya maeneo haya.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ofisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.