Jeshi la majini

tawi la kijeshi lililohusika katika vita vya majini
(Elekezwa kutoka Jeshi la wanamaji)

Jeshi la majini au Jeshi la wanamaji ni kitengo cha pekee cha jeshi la mataifa mengi kilicho tayari kushindana na maadui kwenye maji hasa baharini.

Kundi la manowari la majeshi ya wanamaji ya Marekani, Ufaransa, Italia, uingereza na Uholanzi
Manowari Pyotr Velikiy ya Urusi
Nyambizi Walrus ya Uholanzi
Manowari ya kutega mabomu ya maji HMS Älvborg ya Uswidi
Hovercraft ya Japani
Ndege ya kijeshi kwenye manowari ndege ya Brazil

Linajumlisha askari, manowari, meli za kusaidia manowari, bandari ya pekee na vituo vingine na pia eropleni za vita ya bahari.

Historia

hariri

Ni hasa nchi zenye pwani ya bahari ambako kuna jeshi la pekee la wanamaji. Chanzo katika historia yalikuwa majeshi ya wanamaji ya Karthago, Ugiriki ya Kale na Dola la Roma.

Tangu karne ya 19 Uingereza ilikuwa na jeshi la wanamaji kubwa duniani, na katika karne ya 20 nafasi yake ilichukuliwa na wanamaji wa Marekani hasa, lakini pia wa Urusi.

Marejeo

hariri