Karthago (kwa Kilatini Carthago; kwa Kigiriki Καρχηδών Karchēdōn; katika lugha asilia ya Kifinisia Qart-Hadašt, yaani "mji mpya") zaidi ya miaka 2000 iliyopita ulikuwa mji mkubwa katika Afrika ya Kaskazini karibu na Tunis ya leo nchini Tunisia.

Maghofu ya Karthago.
Mahali pa Karthago na eneo la mamlaka yake mnamo mwaka 264 KK.

Maghofu yake yameorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Historia

hariri

Karthago uliundwa mnamo 814 KK na Wafinisia kutoka pwani ya Shamu na Lebanon kama koloni. Ukakua kuwa mji mkubwa kabisa katika magharibi ya Mediteranea. Ulitawala maeneo ya pwani katika nchi za leo za Libya, Tunisia, Algeria, Moroko, Hispania, Ureno na Ufaransa pamoja na visiwa vikubwa vya Mediteraneo.

Baada ya kuvamiwa na Dola la Roma mwaka 146 KK Karthago ukawa mji wa Kiroma.

Kati ya miaka 439 hadi 533 ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Wavandali katika Afrika ya Kaskazini halafu ukarudi chini ya Bizanti.

Waarabu Waislamu walipovamia Afrika ya Kaskazini mwaka 647 Karthago ulikuwa na kuta na boma imara sana ukafaulu kujitetea hadi mwaka 698 BK.

Baada ya kuteka mji huo Waarabu waliamua kutumia majengo yake kama chimbo la mawe. Nyumba nyingi za mji wa Tunis zimejengwa kwa mawe ya Karthago ya zamani.

Mji wa leo

hariri

Siku hizi Karthago ni mji wenye wakazi 24,216 (2014) na ulio sehemu ya wilaya ya Tunis.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Karthago kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.