Joaquín Lorenzo Villanueva
Joaquín Lorenzo Villanueva Astengo (10 Agosti 1757 – 26 Machi 1837) alikuwa kasisi, mwanahistoria, na mwandishi wa Kihispania.
Alisoma katika Chuo Kikuu cha Valencia na akawa mwanahistoria maarufu wa Kanisa. Aliteuliwa kuwa mhubiri wa kifalme huko Madrid na msimamizi wa kiroho katika kanisa la kifalme.
Mnamo 1823, alihamia Ireland, ambako miaka kumi baadaye alichapisha Phoenician Ireland, kazi iliyolenga kuthibitisha kuwepo kwa makoloni ya Wafinisia wa kale nchini humo. Kazi hiyo ilitafsiriwa kwa Kiingereza mnamo 1837 na Henry O'Brien.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Joaquín Lorenzo Villanueva - letra X". Real Academia Española (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 27 Mei 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |