Valencia (matamshi ya Kihispania: balenthya) ni mji mkuu wa Jimbo la Valencia na mji wa tatu kwa ukubwa nchini Hispania. Kuna wakazi 800,000 mjini penyewe, na takriban milioni 1.6 katika rundiko la mji.

Valencia
Nchi Hispania
Jimbo / Mkoa Valencia
Anwani ya kijiografia 39°28′00″N 0°22′30″W / 39.46667°N 0.37500°W / 39.46667; -0.37500
Kimo mita
Eneo km2 134.65, jiji lote 628.81
Wakazi 791,413
Tovuti rasmi www.valencia.es

Valencia ni mji wa bandari na bandari yake ina nafasi ya tano kati ya bandari za Ulaya kwa kuhesabu idadi ya kontena zinazoshughulikiwa.

Historia

hariri

Valencia ilianzishwa kama koloni la Waroma wa Kale takriban miaka 2000 iliyopita, kwa jina la Valentia Edetanorum.

Baada ya kuporomoka kwa utawala wa Kiroma mji ulikuwa sehemu ya milki ya Wavisigothi.

Mnamo 714 jeshi la Waarabu liliteka Valencia na mabwana wapya walileta walowezi, wakiwa na lugha na utamaduni wao. Walianzisha mifumo bora ya umwagiliaji na kilimo cha mazao mapya pia. Valencia ilikuwa mji mkuu wa milki ya Kiislamu ya Valencia.

Mnamo 1238 mfalme Mkristo Jaume (Yakobo) wa Aragon aliteka mji akaunda Ufalme wa Valencia ulioendelea kuwa sehemu ya pekee ya Milki ya Aragon na baadaye ya Milki ya Hispania. Valencia ilikuwa na sheria zake za pekee kwa karne kadhaa.

Valencia ilikuwa mji mkuu wa Hispania kwa muda mfupi mara mbili; mara ya kwanza mwaka 1812 chini ya mfalme Joseph Bonaparte (mdogo wa Napoleon Bonaparte) halafu tena kati ya miaka 1936 na 1937, wakati wa Jamhuri ya Pili ya Hispania.

Jiografia

hariri

Jiji liko kwenye ukingo wa mto Turia, mdomo wake unapoishia katika Bahari ya Mediterania. Mji wa Kiroma ulianzishwa kwenye kisiwa cha mtoni. Upande wa kusini uko wangwa wa Albufera wenye maji matamu ambao sasa ni hifadhi ya mazingira asilia.

 
Valencia huwa na baridi ya kiasi, usimbishaji kidogo na majira marefu ya joto.

Valencia huwa na tabianchi nusutropiki yaani hakuna baridi kali na majira ya joto ni marefu[1].[2][3]

Halijoto ya wastani kwa mwaka ni °C 23 wakati wa mchana na °C 13.8 usiku.

Januari (mwezi baridi zaidi) halijoto ya mchana huwa kati ya °C 14 - 21, ya usiku kati ya °C 5 hadi 10. Kwenye Agosti, mwezi wa joto, halijoto huwa na °C 28-34 mchana na °C 21 hadi 23 usiku.

Uchumi

hariri

Uchumi wa Valencia hutegemea kwa kiasi kikubwa bandari yake.

Nguzo nyingine ni utalii.

Marejeo

hariri
  1. "Guía resumida del clima en España (1981-2010)". Agencia Estatal de Meteorología (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 7 Novemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Pérez Cueva, Alejandro J. (1994). Conselleria de Vivienda, Obras Públicas y Vertebración del Territorio (mhr.). Atlas climático de la Comunidad Valenciana: 1961-1990 (tol. la 1ª). Valencia: Generalitat Valenciana. uk. 205. ISBN 84-482-0310-0. OCLC 807093628.
  3. Kottek, M.; Grieser, J.; Beck, C.; Rudolf, B.; Rubel, F. (10 Julai 2006). "World Map of the Köppen-Geiger climate classification updated". Meteorol. Z. 15 (3): 259–263. doi:10.1127/0941-2948/2006/0130. Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2009.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Kujisomea

hariri

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Valencia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.