Zoolojia
Zoolojia (kutoka maneno ya Kigiriki ζῷον zóon "mnyama, kiumbe hai" na λόγος logos, "neno, fundisho“) ni tawi la biolojia linalochunguza wanyama, hasa wanyama wenye seli nyingi (metazoa).
Zoolojia linatumia mbinu mbalimbali za kisayansi likichungulia maumbile na miili ya wanyama, michakato ndani ya miili, historia ya mageuko ya spishi za wanyama, jenetiki yao, uenezi wao katika dunia, uhusiano wao na mazingira (ekolojia) na jinsi gani wanahusiana kati yao.
Zoolojia imeunda mfumo wa kupanga wanyama wote kwa vikundi (uainishaji wa kisayansi) na kuendeleza utaratibu huu.
Wanazoolojia kwa kawaida hufuata masomo ya biolojia na kwenye ngazi za juu zinaweka mkazo upande wa elimu ya wanyama. Wanafanya kazi kwenye vyuo vikuu, katika maabara ya makampuni ya madawa, katika bustani za zoo au katika makumbusho.
Viungo vya nje
hariri- media kuhusu Zoolojia pa Wikimedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zoolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |