John Matshikiza
John Matshikiza (26 Novemba 1954 - 15 Septemba 2008) alikuwa mwigizaji wa Afrika Kusini, mkurugenzi wa michezo ya ukumbini,mshairi na mwandishi wa habari.
John Matshikiza | |
---|---|
Amezaliwa | John Matshikiza 26 Novemba 1954 Johannesburg Afrika Kusini |
Amekufa | 15 Septemba 2008 Melville Johannesburg Afrika Kusini |
Kazi yake | Mwigizaji, mshairi na mwandishi wa habari na mkurugenzi wa michezo ya ukumbini |
Wasifu
haririJohn Matshikiza alizaliwa katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini na Todd Matshikiza - mpiga piano mashuhuri wa jazz, mtunzi na mwandishi wa habari na Esme Matshikiza. Kwa sababu ya ubaguzi wa rangi, familia ya Matshikiza ilienda uhamishoni London mnamo 1961. John alikuwa na miaka saba tu walipopanda meli kwenda London. Baade familia ilihamia Lusaka, Zambia ambapo John alimaliza masomo yake na kuchukua digrii ya uchumi na siasa. Alirudi London kusoma katika Central School of Speech and Drama kufundishwa mchezo wa kuigiza. Alipokuwa Uingereza, alifanya kazi kwenye kampuni ya Royal Shakespeare na kampuni ya Glasgow's Citizens Theatre na pia alifanya kazi kwenye runinga na filamu.
Viungo vya Nje
hariri- "John Matshikiza dies in Jo'burg", Mail & Guardian, 16 September 2008.
- John Matshikiza: Poet, actor, journalist and activist The Independent, 20 September 2008.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Matshikiza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |