Juan Carlos Tedesco

Juan Carlos Tedesco (alizaliwa Buenos Aires, 5 Februari 1944) ni msomi wa Argentina na muundaji sera aliyekuwa Waziri wa Elimu, kutoka Desemba 2007 hadi Julai 2009.

Juan Carlos Tedesco: Waziri wa Elimu wa nchi ya Argentina katika mwaka wa 2007

Maisha

hariri

Tedesco alisoma katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires,akafuzu na shahada ya digrii ya Falsafa katika mwaka wa 1968. Alifunza kama Profesa wa Elimu ya Historia katika Vyuo vikuu vya La Plata,El Comahue na La Pampa kabla ya kuandika kitabu chake cha kwanza, Education and Society in Argentina, 1800 - 1945 katika mwaka wa 1972.

 
Juan Carlos Tedesco na Rais wa Argentina Cristina Fernández,2007

Tedesco aliteuliwa kama mtaalamu katika sera za elimu katika mwaka wa 1976 katika Mpango wa Maendeleo katika eneo la Amerika ya Kilatini wa UNESCO. Alikuwa mkurugenzi wa Kituo cha Eneo la Amerika ya Kilatini cha Elimu ya daraja la juu.Kituo hiki kilikuwa cha UNESCO huko Caracas, Tedesco alifanya kazi huko katika miaka ya 1982 hadi 1986 na akawa mkurugenzi wa Kituo cha Elimu Cha Eneo hilo mjini Santiago katika miaka ya 1986 hadi 1992. Mateso na ukandamizaji wa walimu na wanafunzi nchini Argentina katika miaka ya udikteta ilimfanya Tedesco kushiriki katika uandishi wa kitabu cha kutatua shida hiyo,The Authoritarian Educational Agenda,akikiandika na Cecilia Braslavsky katika mwaka wa 1983.

Umaarufu wake ulimpa cheo cha Mkurugenzi wa IBE jijini Geneva,cheo alichokuwa nacho hadi mwaka wa 1997, na kuwa mkuu wa UNESCO ya Buenos Aires hadi mwaka wa 2004. Tedesco alirudi katika kufunza,akigawanya muda wake ili kufunza katika Universidad de San Andrés na Chuo Kikuu cha kitaifa cha Tres de Febrero,vyote vikiwa nje ya Buenos Aires. Aliteuliwa na Waziri wa Elimu,Daniel Filmus katika Tume ya Kufunza Walimu.Daniel Filmus alimbadilisha Naibu wa Waziri Albert Sileoni na Tedesco hapo mwezi wa Aprili 2006.

Uchaguzi wa 2007 wa Filmus kama Seneta wa jiji la Buenos Aires na Seneta Cristina Kirchner kama Rais wa Argentina, ulisababisha kuapishwa kwa Tedesco kama Waziri wa Elimu katika 10 Desemba ,2007. Baada ya kushindwa katika mwazi wa 28 Juni 2009, uchaguzi mdogo na kuchanganywa kwa mawaziri, alifutwa kazi huku akibadilishwa 20 Julai na Sileoni. Tedesco alifanywa Mkurugenai Mkuu wa Kituo cha Mikakati ya kuendeleza Elimu nchini Argentina na Rais mwenyewe.

Vitabu alivyoandika

hariri
  • Education and Society in Argentina, 1800 - 1945 katika mwaka wa 1972.
  • The Authoritarian Educational Agenda,akikiandika na Cecilia Braslavsky katika mwaka wa 1983.

Marejeo

hariri
  1. La CapitalLugha ya Kihispania
  2. La CapitalLugha ya Kihispania
  3. La CapitalLugha ya Kihispania

Viungo vya nje

hariri
  1. Clarín (7/20/2009Lugha ya Kihispania