Julia Teresa Tallon
Julia Teresa Tallon (alijulikana kwa jina la kitawa Mary Teresa; 6 Mei 1867 – 10 Machi 1954) alikuwa mtawa Mmarekani katika Shirika la Msalaba Mtakatifu, ambaye alianzisha shirika la "Watembeleaji wa Parokia wa Maria Mkingiwa Dhambi Asili".[1]
Tallon alizaliwa na wahamiaji wa Kiayalandi huko New York City na alijiunga na maisha ya kitawa huko Indiana licha ya pingamizi za familia yake.
Tallon alipewa jina la Mtumishi wa Mungu tarehe 20 Februari 2013 chini ya Papa Benedikto XVI, wakati mchakato wa kutangazwa mwenye heri ulipoanzishwa katika Jimbo kuu la New York.
Marejeo
hariri- ↑ "Mother Julia Teresa Tallon". Saints SQPN. 26 Februari 2016. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |