Juma Hamad Omar ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CUF. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Ole kwa miaka 20152020. [1]

Juma Omar alipata elimu yake ya msingi Skuli ya msingi Ngambwa (1960-1968) baadae kujiunga na elimu ya sekondari Fidel Castro (1969-1972) baadae elimu ya sekondari ya juu Lumumba (1973-1974).

Juma Omar alipata shahada yake ya mwanzo ya ualimu akibobea katika somo la fizikia chuo kikuu cha Dar es Salaam (1975-1978) na baadae kujiunga na chuo kikuu cha Reading (1980-1981) na kuchukua shahada ya uzamivu.

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania Ilihifadhiwa 25 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., iliangaliwa Mei 2017