Chama cha Wananchi
Chama cha Wananchi au Civic United Front (CUF) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania. CUF iliwasilishwa rasmi mnamo Januari 1993.
CUF ilianzishwa mwaka 1992 kutokana na maungano ya shirika mbili. Hizi zilikuwa
- KAMAHURU kikundi cha kupambania demokrasia kwenye visiwa vya Unguja na Pemba
- Civic Movement iliyokuwa kundi la kupigania haki za binadamu la Tanzania bara.
Kama ilivyo katika vyama vingine vipya vya Tanzania, viongozi wengi waliwahi kuwa wanachama wa CCM.
Uongozi
hariri- Mwenyekiti : Profesa Ibrahim Lipumba
- Makamu Mwenyekiti: Machano Khamis Ali
- Katibu Mkuu:
Kura
haririCUF ilishiriki katika chaguzi za kitaifa pia za Zanzibar.
Ilifaulu vizuri kwenye visiwa vya Zanzibar, hasa Pemba, lakini ilibaki hafifu Tanzania bara. Hata hivyo ni chama cha pili cha upinzani katika bunge la Tanzania chenye wabunge 30 kati ya 324 kwa jumla.
Zanzibar
haririKatika kura za Zanzibar CUF ilifikia tokeo rasmi la 49.76% mwaka 1994 na 46.07% mwaka 2000. Watazamaji waliona kila kura ilikuwa na kasoro na CUF haikukubali matokeo ikidai ya kwamba serikali ya SMZ ilibadilisha matokeo ya kweli.
Baada ya uchaguzi wa 2005 CUF ilikuwa na wabunge 19 katika bunge la Zanzibar.