Kenya National Bureau of Statistics

(Elekezwa kutoka KNBS)

Kenya National Bureau of Statistics (kifupi: KNBS; Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya) ni taasisi ya serikali ya Kenya iliyopewa kazi ya kutunza takwimu za nchi hii

Sheria ya Takwimu (Statistics Act 2006) inataja wajibu wake kama ifuatavyo:

  • kuwa taasisi kuu ya serikali inayokusanya data, kuzitathmini na kusambaza taarifa zake
  • kutunza data rasmi
  • kuendesha sensa ya kitaifa kila baada ya miaka 10
  • kujenga na kutunza mkusanyiko wa data za jamii na uchumi
  • kufuata mbinu sanifu katika ukusanyaji na usambazaji wa data
  • kupanga, kuruhusu na kusimamia miradi yote ya takwimu ndani ya mfumo wa takwimu wa taifa

KNBS ilitanguliwa na idara ya takwimu ya serikali. Sheria ya 2206 iliunda taasisi mpya yenye kiwango kikubwa cha madaraka ya kuendesha mambo yake bila kutegemea maagizo ya mara kwa mara kutoka serikalini.

Viungo vya Nje

hariri