Kwanza Unit
Kwanza Unit (vilevile KU Crew) lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1990 kwa muunganiko wa makundi kadhaa na wasanii wa rap. Awali walikuwa wanarap kwa Kiingereza, lakini baadaye wakawa wanatumia Kiswahili vilevile.
Kwanza Unit | |
---|---|
Kuanzia kushoto K-Singo (KBC), D-Rob, Fresh G, Y-Thang, Eazy B., Zavara | |
Taarifa za awali | |
Chimbuko | Dar es Salaam Tanzania |
Miaka ya kazi | 1990– |
Ameshirikiana na | King Kikii |
Wanachama wa zamani | |
Chief Rhymson(Ramadhan A. Mponjika) KBC aka K-Singo (Kiba Cha Singo) Adili "Nigga One" Kumbuka - amefariki 1993
Papa Sav (Makanga Lugoe) Abbas Maunda Balbo Baraka Fresh-G Y-Thang Gaddy Groove |
Historia
haririWanachama waanzilishi wa Kwanza Unit ikiwa ni pamoja na makundi matatu makuu ya hip-hop kwa kipindi hiko – Villain Gangsters, Raiders Posse, na Tribe-X. Kwa mujibu wa Rhymson, mwanachama mwanzilishi wa kundi la Villain Gangsters, lengo la kuanzisha Unit ilikuwa ilikuwa kuifanya Tanzania kama "taifa la hip hop." Vilevile walitazamia kuondoa vijana katika maisha ya mtaani, hasa yale ya hali duni na kuweza kujitegemea na kuondokana na hali hiyo kabisa. [1]
Mpango wa Kwanza Unit ulikuwa kufuata nyayo za Afrika Bambaataa, Mmarekani Mweusi aliyeanzisha hip-hop ambaye pia ndiye aliyejenga Universal Zulu Nation. Kama alivyofanya Afrika Bambaataa, Kwanza Unit walitaka kuchochea maadili ya taifa. Kundi lilianzisha kama kikundi chao cha utamaduni wa Kikwanza ambao ulilenga mashabiki, wasanii na yeyote yule aliyekuwa anaunga mkono maazimio yao ndani na nje ya Tanzania. Hip-hop ilitakiwa hasa iwe kiunganishi cha taifa la Wakwanza ambalo lilikuwa na miiko yake katika maisha ikiwa ni pamoja na tamaduni, thamani, na malengo yake yenyewe. Kwanza Unit inawakilisha muundo / aina ya hip-hop ya kizalendo. Kama vile jinsi Afrika Bambaataa alivyothubutu kuchochea harakati za kupinga ubaguzi na dhulma huko nchini Marekani, Kwanza Unit walitaka kuwa "alama ya mashujaa wanaopinga dhulma". Msisitizo wao ulikuwa si tu katika kupinga ubaguzi, bali pia kutambulika na mapambano dhidi ya dhulma katika nafasi za kazi.[2]
Wakati wanatamba katika miaka ya 1990, Kwanza Unit walikemea sana ubaguzi katka kazi, badala ya kufokasi katika masuala ya ubaguzi wa rangi peke yake. [3] Kwanza Unit walijaribu kutengeneza muziki wao bila ya kutumia hadithi za fujo, lugha chafu, na taswira zenye umaarufu kupitiliza, ingawaje dhamira hizo ni za kawaida katika muziki wa rap ya Marekani ambapo wao ndipo walipopata athira yao. Lugha walizokuwa wanazitumia katika rap uap ziliakisi nafasi kubwa katika jamii na itikadi ndani ya Tanzania.[4]
Kwanza Unit waliweza kupata umaarufu kimataifa. Waliwahi kutumbuiza mara mbili mjini Nairobi, Kenya na mwaka wa 1998 walialikwa nchini Nigeria lakini hawakuweza kwenda kwa sababu fulani-fulani.[5]
Albamu ya kwanza ya Kwanza Unit iliitwa jina lao ilitoka mwaka 1994 na tepu yao ya pili ilitoka mwaka uliofuata Tropical Techniques ilitoka mwaka uliofuata. Albamu ya tatu, Kwanzanians ilitolewa mwaka 1999, ikiwa katika tepe na CD. Kibao cha Msafiri, kutoka katika albamu yao ya tatu, Kwanzanians.
Kama jinsi walivyo-wanachama wa makundi mengine ya muziki wa hip-hop duniani, Kwanza Unit walipitia magumu mengi ambayo yanafanana kwa kiasi kikubwa na muziki wa Marekani. Japokuwa muziki wa Marekani umeleta hamasa kubwa katika harakati nzima ya muziki wa hip hop nchini Tanzania, vilevile ilizua balaa la wasiwasi wa kuharibikiwa kwa maadili na utamaduni nchini vilevile. Mmoja kati ya wanachama wa Kwanza Unit alisikika akisema ya kwamba "wakati tunangeneza albamu yetu tuliweka makubaliano ya kwamba hakuna mmmoja wetu kufa kabla ya kutoa kazi yetu..." lakini baadaye ikagundulika ya kwamba "[m]iezi mitatu baadaye [Nigga One] amekufa katika ajali ya gari."[6] Hii inaashiria udokezo mkubwa wa muundo wa hip-hop ya Marekani, ka,a vile Tupac Shakur na The Notorious B.I.G., ambap walikufa wakiwa vijana kabisa. Japokuwa Nigga One hajauawa, ukweli wa kwamba makubaliano ya kuwa hai ulionesha elementi hatari kwa hip-hop. Isitoshe, matumizi makubwa ya Kiingereza katika hip-hop yalizua kitendawili kwa Kwanza Unit. Awali, rap ilikuwa inafanywa kwa Kiingereza tu, lakini polepole ikawa inabadilika kwa Kiswahili, huku Kwanza Unit na wanamuziki wengine wa Tanzania walianza kusimamia kazi zao wenyewe.[7]
Rhymson mmoja wa waanzilishi wa kundi, alishuhulikia kueneza neno zuri juu ya rap katika mahojiano kadha wa kadha. Hip-hop si kwa ajili ya "wahuni" tu na vilevile kuna ujumbe mzito wa kusikiliza. "Tatizo kubwa ambalo linazunguka katika jamii kwa ujumla inadhani ya kwamba rap ni kwa ajili ya wahuni. Hili pia linapelekea kutia ugumu wa kuchezwa katika maredio. Vyombo vya habari vinahitaji ujumbe sahihi. Jambo ambalo kwangu ni chanya linaweza lisiwe chanya kwako. Iwapo polisi watanitenda vibaya naweza kulaani ili nipunguze machungu yangu baada ya kukerwa na polisi. Kama nitasema hayo katika mashairi, ile kisanii zaidi, haina ulazima redioni wasema ujumbe huu ni chanya au la. Wanaweza kusema ni hasi kimtazamo wao, kwa sababu kila mtu ana haki ya kufikiria watakavyo. Katika hip hop naweza kuelezea mtazamo wangu kwa kukupa changamoto, hivyo basi siku inayofuata unakuja kwangu na kusema: Una maana gani unaposema hivyo?" [8]
Wanachama wa KU Crew
haririKwanza Unit lilikuwa na wanachama kadhaa na mabadiliko kadha wa kadha. Wanachama hao ni pamoja na:
- Chief Rhymson (Ramadhan A. Mponjika)
- KBC aka K-Singo (Kibacha Singo)
- Adili "Nigga One" Kumbuka – amekufa 1993
- D-Rob (Robert Mwingira) – amekufa 2001
- Eazy-B (Bernard Luanda)
- Papa Sav (Makanga Lugoe)
- Abbas Maunda
- Balbo Mwingira(Marehemu)
- Baraka
- Fresh-G(Godfrey Koshuma)
- Y-Thang
- Gaddy Groove
Vilevile kuna mzunguko mkubwa wa wanachama wanaotajwa kama Kwanza Unit Foundation au Kwanzanians' - Wakwanza.
Kwanza Unit Foundation:
- Bugzy Malone (Edward Margat)
- Ndoti Mwingira
- Richard Mwingira
- Totoo
- Base One aka KK (Khalid Kumbuka)
- Lenana
- Sundeo
Diskografia
hariri- Kwanza Unit - 1994
- Tropical Teqniks - 1996
- Kwanzanians - 2000
Tabihi
hariri- ↑ Zavara Mponjika, katika vijambo TV, NY Marekani. http://darslamproductions.blogspot.com/2012/05/zavara-mponjika-muanzilishi-wa-kwanza.html
- ↑ Lemelle, Sidney J. "'Ni wapi Tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha." In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
- ↑ Lemelle, Sidney J. “‘Ni wapi Tunakwenda’: Hip Hop Culture and the Children of Arusha.” In The Vinyl Ain’t Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
- ↑ "Language choice and hip hop in Tanzania and Malawi | Popular Music and Society | Find Articles at BNET.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-12. Iliwekwa mnamo 2017-05-09.
- ↑ "Rockers Magazine Tanzania". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-02-20. Iliwekwa mnamo 2017-05-09.
- ↑ Kasumba, Lee. 20 February 2008. "Emcee Africa – The Battle Chronicles #2: Tanzania – Mzuka!" www.africanhiphop.com. http://www.africanhiphop.com/index.php?module=subjects&func=viewpage&pageid=286. Accessed 7 March 2008.
- ↑ Malm, Krister and Monika Sarstad. 1997. "Rap, Ragga and Reggae in Dar es Salaam: Kwanza Unit." http://www.musikmuseet.se/mmm/africa/ku.html. Accessed 7 March 2008.
- ↑ [1]
Marejeo
hariri- Lemelle, Sidney J. "'Ni wapi Tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha." In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
Viungo vya Nje
hariri- www.xs4all.nl Ilihifadhiwa 20 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
- Kwanza Unit profile Ilihifadhiwa 25 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine.
- katika HashLonga blogu