Kafue (mto)
Mto Kafue ni kati ya matawimto makubwa ya mto Zambezi; una chanzo chake kusini mwa mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia. Urefu wa mwendo wake ni takriban kilomita 960.
Chanzo | Kaskazini mwa Zambia karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Mdomo | mto Zambezi mpakani na Zimbabwe |
Nchi | Zambia |
Urefu | 960 km |
Kimo cha chanzo | 1,350 m |
Mkondo | 320 m³/s wastani |
Eneo la beseni | km² 155,000 |
Miji mikubwa kando lake | Kafue, Mazabuka |
Inajiunga na Zambezi karibu na mji wa Chirundu (Zimbabwe).
Ni kati ya mito mikubwa ya Zambia na maji yake husaidia sana kilimo pamoja na kutengeneza umeme.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kafue (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |