Kaldera ni shimo kubwa ya mviringo iliyotokea wakati volkeno inaporomoka ndani yake baada ya mlipuko.

Kaldera hutokea kama chumba cha magma chini ya volkeno kimetoa nje yaliyomo yake yote na kuacha uwazi mkubwa (nafasi) ardhini. Mlima juu yake unaporomoka ndani ya nafasi hiyo na kuacha shimo juu yake: kaldera. Neno la kaldera lina asili ya Kihispania kumaanisha "sufuria" au "bakuli".

Kaldera ikijaa maji huwa ziwa kubwa la kasoko.

Kaldera inaweza kupatikana ndani ya kelele cha mlima. Kama kuporomoka kulitokea vikali sana mara nyingi mlima mwenyewe ulipotea ukaacha tu dalili za ukingo wake.

Kaldera kubwa kabisa duniani yenye ukingo usiovunjika au kukatika ni Ngorongoro (Tanzania) yenye kipenyo wa 27 km.

Kaldera inaweza kuonekana kama kasoko ya volkeno lakini historia yake ni tofauti.

Kaldera ya Ngorongoro penye hifadhi za wanyamapori
Kaldera ya Santorini (Ugiriki) imefunikwa na bahari ya Mediteranea. Mabaki ya ukingo yanaonekana kama mviringo wa visiwa