Kasoko ya volkeno

Kasoko ya volkeno (pia: kreta kutoka gir./ing. crater) ni shimo kubwa katika mlima wa volkeno.

Kasoko ya volkeno Mount St. Helens (Marekani) baada ya mlipuko wa 1980 - sehemu ya ukingo umepotea

Zaha na gesi za joto zinapotoka ardhini kuwa volkeno husababisha kutokea kwa kasoko. Milima ya volkeno huwa na kasoko kwenye kelele mara nyingi pia na kasoko kando.

Kasoko za volkeno inayolala au iliyozimika mara nyingi hujaa maji kuwa "ziwa la kasoko".

Shimo linaweza kuonekana kubwa zaidi kama volkeno imeporomoka ndani yake yenyewe halafu huitwa "kaldera".