Kanda ya Kati, Malawi
Kanda ya Kati ni moja ya kanda tatu za kiutawala nchini Malawi. Idadi ya wakazi ilkuwa 7,523,340 kwenye mwaka 2018. Eneo lake ni kilomita za mraba 35,592.
Makao makuu yako Lilongwe, ambayo pia ni mji mkuu wa taifa. Kanda hii inapakana na nchi jirani za Zambia na Msumbiji. Kabila la Wachewa ni sehemu kubwa zaidi ya wakazi.
Jiografia
haririKanda ya Kati inapakana upande wa kaskazini na Kanda ya Kaskazini, upande wa mashariki na Ziwa Nyasa (Ziwa Malawi), upande wa kusini-mashariki na Kanda ya Kusini, kwenye kusini-magharibi na Msumbiji, na upande wa mashariki na Zambia.
Kanda ya Kati iko kwenye ukingo wa magharibi wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Ziwa Nyasa linachukua sehemu kubwa ya bonde la ufa, na uwanda mwembamba unapita kwenye ufuo wake wa magharibi. Sehemu kubwa ya eneo hilo iko kwenye tambarare, inayojulikana kama Nyanda za Juu za Kati au Uwanda wa Lilongwe wenye kilomita za mraba 23,310.[1] Mito ya Dwangwa, Bua, na Lilongwe inakusanya maji kwenye nyanda za juu, ikitiririkia mashariki kuelekea Ziwa Nyasa.
Mpaka wa kusini-magharibi wa mkoa huo ni wa milima, ikijumuisha mwisho wa safu ya Kirk na Mlima Dedza (m 2,198).
Utawala
haririKati ya wilaya 27 nchini Malawi, 9 ziko ndani ya Kanda ya Kati nazo ni:
Marejeo
hariri- ↑ "Central Region Plateau." Encyclopaedia Britannica online. Accessed 1 September 2019.