Kanisa la Kisiria la Kiorthodoksi la Malankara


Kanisa la Kisiria la Kiorthodoksi la Malankara ni mojawapo kati ya yale ya Waorthodoksi wa Mashariki.

Ishara ya Umalankara.

Inasemekana asili yake ni kusini mwa India mwaka 52 BK kwa juhudi za Mtume Thoma.

Kihistoria, Wakristo wa huko walikuwa na ushirika na Kanisa la Asiria.

Walipofikiwa na wale wa Ureno katika karne ya 16wengi hawakupenda kulazimishwa wafuate mapokeo ya Ukristo wa Mashariki, hivyo wakaanza kufarakana.

Baadhi wakakimbilia msaada wa Kanisa la Kiorthodoksi la Siria na kujiunga nalo (1665).

Waliohama Kerala katika karne ya 20 walieneza imani na mapokeo yao sehemu mbalimbali duniani.

Kwa jumla wako milioni mbili unusu.

Makao makuu yako Kottayam.

External links hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kisiria la Kiorthodoksi la Malankara kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.