Mtume Thoma
Thoma (au Didimo, yaani Pacha) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India.
Mitume wa Yesu |
---|
|
Inawezekana kwamba sababu yake ni kazi za utume alizozifanya huko hadi kifodini chake huko Chennai mwaka 72 (kaburi lake huonyeshwa katika mji huo wa Tamil Nadu). Mpaka leo kusini-magharibi mwa Bara Hindi wako wanaojiita "Wakristo wa Thoma" ambao kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine wa mbali.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na madhehebu mengine mbalimbali kama mtakatifu.
Chanzo cha umaarufu wake
haririAlikuwa mtu mwenye tabia ya pekee iliyomvutia umaarufu hadi leo. Hasa alielekea kukata tamaa, kupinga hoja na kutosadiki kwa urahisi, kama alipokataa kusadiki ushahidi wa mitume wenzake juu ya ufufuko wa Yesu[2].
Mfano mmojawapo ni pale ambapo katika karamu ya mwisho alimjibu Yesu kwa wasiwasi: "Bwana, hatujui uendako; tutajuaje basi njia?" (Yoh 14:5). Ndipo Yesu alipojitambulisha kama njia: "Mimi ndimi njia, ukweli na uzima" (Yoh 14:6).
Hata hivyo, Injili ya Yohane ambayo ndiyo inayomzungumzia zaidi katika Biblia ya Kikristo, inaripoti jibu lake la mwisho kwa Yesu mfufuka kama ifuatavyo (Yoh 20:28): "Bwana wangu na Mungu wangu!" Katika Injili hakuna ungamo la wazi zaidi la umungu wa Yesu Kristo.
Hata hivyo, Yesu alimuambia wana heri zaidi wanaosadiki bila kuona kwanza. Na ndilo lengo la Yohane katika kuandika Injili yake: kuwafanya wasomaji wasioweza tena kumuona Yesu wamuamini na hivyo kupata uzima wa milele.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya nje
hariri- St. Thomas the Apostle Ilihifadhiwa 6 Juni 2012 kwenye Wayback Machine.
- The Life of St. Thomas the Apostle of Jesus Christ Ilihifadhiwa 17 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine.
- Apostle in India, The tomb of the Apostle
- Mylapore santhomechurch built over the tomb of St. Thomas Ilihifadhiwa 3 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- St. Thomas Indian Orthodox Church – Greater Washington
- A.E. Medlycott, India and the Apostle Thomas, London 1905 (e-text)
- Niranam Valiyapally and St. Thomas Ilihifadhiwa 1 Juni 2005 kwenye Wayback Machine.
- St.Thomas Christian History and Culture
- The Nasrani Syrian Christians Network
- Thomasine Church Ilihifadhiwa 11 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Official Site of the Malankara Mar Thoma Syrian Church Ilihifadhiwa 10 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Mar Thoma Churches all over the world Ilihifadhiwa 10 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.
- Passages to India
- Orthodox Church Portal
- Indian Orthodox Church
- Holy, Glorious Apostle Thomas Orthodox icon and synaxarion for 6 Oktoba
- Apostle Thomas—Synaxis of the Holy Apostles Orthodox icon and synaxarion for 30 Juni
- Icon of the Mother of God Arapet (Arabian) Orthodox icon and synaxarion for 6 Septemba
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Thoma kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |