Kaptura ni vazi lililovaliwa na wanaume na wanawake juu ya eneo la nyonga yao, likizunguka kiuno na kugawanyika ili kufikia sehemu ya juu ya miguu, wakati mwingine hupanda magoti lakini si kufunika urefu mzima wa mguu.

Mchoro wa kaptura.
Skauti huwa wamevaa kaptura kama sehemu ya sare yao.

Ni toleo la kufupishwa kwa suruali, ambalo hufunika mguu mzima, ndiyo sababu kwa Kiingereza huitwa "shorts", kwa kufa linafanana na suruali fupi huku tofauti ikiwa kuwa inaanzia kwa kiuno hadi kwa magoti. Suruali ndefu nayo huanzia kwa kiuno hadi miguuni.

Kwa kawaida huvaliwa katika hali ya hewa ya joto au katika mazingira ambapo faraja na mtiririko wa hewa ni muhimu kuliko ulinzi wa miguu.

Katika jamii nyingi za Afrika, vazi hilo ni la wavulana wadogo huku wakubwa wao na wazee wakivaa suruali ndefu. Nchi za Amerika na Uingereza pia zilikuwa na mitindo hiyo ya kuwapa wavulana kaptura (suruali fupi) huku wakipewa suruali ndefu walipokomaa. Haya yalifanyika katika karne ya 18 lakini kwa sasa vazi hili limekuwa la wote.

Suruali fupi hutumika hasa kwa michezo ambapo wanaspoti hulivalia vazi hili maana lawawezesha kucheza bila kuhisi kana kwamba wamebanwa na vazi hili. Hata hivyo kwa wanaofanya kazi katika kampuni, kaptula haifai lakini wafaa uvae suruali ndefu litakalodumu kwa muda mrefu.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaptura kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.