Skauti

mwanachama wa harakati ya Skauti

Skauti (kutoka neno la Kiingereza "scout") ni mtoto, kijana au msichana anayewajibika katika chama cha kimataifa, akivaa sare kama ya askari mdogo na kukaa katika safu.

Viongozi wakipokea mtoto katika chama cha skauti huko Mexico City, Mexico.

Pia ni chama kisicho cha kiserikali kinachomjenga kijana katika maadili mema na ya kujituma na kusaidia watu katika maisha yao.

Chama hicho hakibagui vijana kwa msingi wa jinsia, umri, dini, rangi wala kabila.

Skauti huhitajika kuwepo kwa kila shule za sekondari duniani.

Mwanzilishi wa uskauti duniani (1907) alikuwa Robert Baden-Powell (18571941) kutoka Uingereza. Lengo lake lilikuwa kusaidia vijana kukua vizuri pande zote (mwili, nafsi na roho) ili hatimaye wawe raia wema katika jamii. Leo hii wako skauti milioni waliounganisha katika makundi na vyama vingi; idadi kubwa aidi nni wanachama katika Shirika la Harakati za Skauti Duniani linalounganisha skauti milioni 57[1] kote duniani.

Kanuni za skauti hariri

  • 1. skauti ni mwaminifu.
  • 2. Skauti ni mzalendo kamili.
  • 3. Skauti ni mtu wa kufaa na kusaidia wengine.
  • 4. Skauti ni rafiki kwa wote na ndugu kwa kila mtu aliye skauti na asiye skauti.
  • 5. Skauti ni mwenye adabu kamili.
  • 6. Skauti ni mwenye huruma na viumbe hai.
  • 7. Skauti ni mtiifu kamili.
  • 8. Skauti ni mchangamfu daima hakati tamaa.
  • 9. Skauti ni mlinzi wa mali zake na za wengine.
  • 10.Skauti ni safi katika mawazo, maneno na matendo yake pia.

Marejeo hariri