Tatata
(Elekezwa kutoka Kapurapunda)
Tatata | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tatata mbavu-nyeupe (Batis molitor)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 20:
|
Tatata au kapurapunda ni ndege wadogo wa jenasi Batis katika familia Platysteiridae wanaotokea Afrika chini ya Sahara. Zamani waliainishwa katika familia Muscicapidae. Takriban spishi zote zina kinyago cheusi, utosi kijivu, mgongo kijivu au mweusi, tumbo jeupe na kidari chenye mlia mweusi au kahawiachekundu. Dume ana nyeusi zaidi na jike ana nyekundu zaidi. Hula wadudu na hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka. Jike huyataga mayai 1-4.
Spishi
hariri- Batis capensis, Tatata Kusi (Cape Batis)
- Batis crypta, Tatata Mweusi (Dark Batis)
- Batis diops, Tatata wa Ruwenzori (Ruwenzori Batis)
- Batis erlangeri, Tatata Kichwa-cheusi Magharibi (Western Black-headed Batis)
- Batis fratrum, Tatata wa Woodward (Woodward's Batis)
- Batis ituriensis, Tatata wa Ituri (Ituri Batis)
- Batis margaritae, Tatata wa Margarita (Margaret's au Boulton's Batis)
- Batis minima, Tatata wa Gaboni (Gabon au Verreaux's Batis)
- Batis minor, Tatata Kichwa-cheusi Mashariki (Eastern Black-headed Batis)
- Batis minulla, Tatata wa Angola (Angola Batis)
- Batis mixta, Tatata Mkia-mfupi (Forest au Short-tailed Batis)
- Batis molitor, Tatata Mbavu-nyeupe (Chinspot Batis)
- Batis occulta, Tatata wa Lawson (West African Batis)
- Batis orientalis, Tatata Utosi-kijivu (Grey-headed Batis)
- Batis perkeo, Tatata Mdogo (Pygmy Batis)
- Batis poensis, Tatata wa Bioko (Fernando Po Batis)
- Batis pririt, Tatata wa Namibia (Pririt Batis)
- Batis reichenowi, Tatata wa Reichenow (Reichenow's Batis)
- Batis senegalensis, Tatata Magharibi (Senegal Batis)
- Batis soror, Tatata-pwani (Pale Batis)
Picha
hariri-
Tatata kusi
-
Jike wa tatata wa Woodward
-
Tatata wa Margarita
-
Tatata kichwa-cheusi mashariki
-
Tatata mkia-mfupi
-
Tatata utosi-kijivu
-
Tatata wa Namibia
-
Tatata magharibi
-
Tatata-pwani