Karen Christence Blixen-Finecke (jina la kiuandishi alilotumia kwenye nchi zinazozungumza Kiingereza: Isak Dinesen) (Rungsted/ Denmark 17 Aprili 1885 - 7 Septemba 1962) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijerumani, Osceola na Pierre Andrézel.

Karen Blixen (1913)

Aliishi Kenya -wakati ule: Afrika ya Mashariki ya Kiingereza- kati ya 1913 hadi 1931 akiongoza shamba la kahawa karibu na mji wa Nairobi. Eneo la shamba lake la zamani hadi leo laitwa "Karen" ni kitongoji cha Nairobi.

Aliandika kumbukumbu ya maisha yake Kenya na kitabu hiki kikawa msingi wa filamu "Out of Africa". Huko Denmark alijulikana sana kwa kazi yake iitwayo Seven Gothic Tales.

Early years hariri

Karen Blixen na kaka yake Thomas kwenye shamba la familia huko Kenya kwenye miaka ya 1920

Karen Dinesen alizaliwa Rungstedlund, kaskazini mwa Copenhagen. Baba yake, Wilhelm Dinesen (1845–1895), alikuwa ni mwandishi na ofisa wa kijeshi toka familia ya wamiliki wa mashamba ya Jutland yenye uhusiano wa karibu na ufalme, kanisa na siasa za mrengo wa kulia. Mama yake, Ingeborg Westenholz (1856–1939), alitoka kwenye familia tajiri inayofanya biashara. Karen Dinesen alikuwa ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa kike na wawili wa kiume. Mdodo wake wa kiume, Thomas Dinesen, alipata tuzo ya Victoria Cross wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.[1] Dinesen was known to her friends as "Tanne".


Vitabu hariri

  • Eneboerne (The Hermits), Agosti 1907, kilichapishwa kwa jina la Tilskueren kwa jina lake la uandishi Osceola
  • Pløjeren (The Ploughman), Oktoba 1907, kwa jina la Gads danske Magasin,akitumia jina la Osceola
  • Familien de Cats (The de Cats Family), Januari 1909, kwa jina la Tilskueren akitumia jina la Osceola
  • Sandhedens hævn – En marionetkomedie, Mei 1926, akitumia jina la Karen Blixen-Finecke
  • Seven Gothic Tales (1934 nchini Marekani, 1935 nchini Denmark)[2]
  • Out of Africa (1937 Denmark na Uingereza, 1938 nchini Marekani)
  • Winter's Tales (1942)[3]
  • The Angelic Avengers (1946)[4]
  • Last Tales (1957)[5]
  • Anecdotes of Destiny (1958) (pamoja na Babette's Feast)
  • Shadows on the Grass (1960 Uingereza na Denmark, 1961 Marekani)[6]
  • Ehrengard (baada ya kufa 1963, Marekani)[7]
  • Carnival: Entertainments and Posthumous Tales (baada ya kufa 1977, Marekani)[8]
  • Daguerreotypes and Other Essays (baada ya kufa 1979, Marekani)[9]
  • On Modern Marriage and Other Observations (baada ya kufa 1986, Marekani)[10]
  • Letters from Africa, 1914–1931 (baada ya kufa 1981, Marekani)[11]
  • Karen Blixen in Danmark: Breve 1931–1962 (baada ya kufa1996, Denmark)
  • Karen Blixen i Afrika. En brevsamling, 1914–31 i IV bind (baada ya kufa 2013, Denmark)[12]

Marejeo hariri

  1. C. Brad Faught, 'The Great Dane and her hero brother', National Post, Toronto, 4 May 2002.
  2. Fall, John Updike; John Updike's New Novel, Roger's Version, Will Be Published In The. "'SEVEN GOTHIC TALES': THE DIVINE SWANK OF ISAK DINESEN", The New York Times, 23 February 1986. 
  3. Spurling, Hilary. "Book choice: Winter's Tales", Telegraph.co.uk. (en) 
  4. THE ANGELIC AVENGERS by Isak Dinesen | Kirkus Reviews (in en-us). 
  5. LAST TALES by Isak Dinesen | PenguinRandomHouse.com (in en-US). 
  6. Shadows on the Grass by Isak Dinesen (en).
  7. "Ehrengard | Karen Blixen", Adelphi Edizioni. (it-it) 
  8. Carnival. 
  9. Daguerreotypes and Other Essays. 
  10. Summary/Reviews: On modern marriage, and other observations /. www.buffalolib.org (in English) (St. Martin's Press). 1986. ISBN 9780312584436. Archived from the original on 2019-03-31. Retrieved 15 April 2017. 
  11. The British Empire, Imperialism, Colonialism, Colonies.
  12. Karen Blixen i Afrika : en brevsamling, 1914–31 – Karen Blixen | bibliotek.dk (da).


Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karen Blixen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.