Karim Achahbar (alizaliwa 3 Januari 1996) ni mwanasoka wa kulipwa ambaye anacheza kama mshambuliaji wa timu ya akiba ya Chamois Niortais. Mzaliwa wa Ufaransa, aliiwakilisha Moroko katika viwango vya kimataifa ngazi ya vijana.

Maisha ngazi ya klabu

hariri

Mshambuliaji huyu alijiunga na EA Guingamp mwaka wa 2014. Alichangia upatikanaji wa taji la EA Guingamp la 20132014 la Coupe de France kwa kucheza dhidi ya FC Bourg-Péronnas mnamo 5 Januari 2014 na akacheza mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Montpellier HSC mnamo 27 Septemba 2014.

Mnamo 18 agosti 2015, alitolewa kwa mkopo na kuelekea Vendée Luçon.[1]

Kazi ya kimataifa

hariri

Achahbar alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Moroko ya wenyw umri chini ya miaka 17 kwenye Kombe la Dunia la FIFA la wenye umri chini ya miaka 17 la mwaka 2013. Katika shindano hili, alicheza michezo 4 na kufunga mabao 3.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karim Achahbar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Guingamp prête Karim Achahbar à Luçon (National)", L'Equipe, 18 August 2015. Retrieved on 21 August 2016. (French)