Katibu

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Katibu (kutoka neno la Kiarabu) ni mtu anayefanya kazi ya kuandika, kwa mfano kumbukumbu za mikutano.

Anaweza pia kuwa na jukumu la kupanga na kuhifadhi maandishi ya shirika, chama au kampuni.

Neno Katibu pia lina maana ya mtu katika shirika anayepatiwa kazi maalumu.

Katibu kama msaidizi

hariri

Katika shirika au kampuni, katibu huwa msaidizi ofisini. Majukumu yake huhusiana na uandishi wa kumbukumbu, kufaili hati za ofisi na kupanga ratiba za wakuu wake. Majukumu hutofautiana kulingana na kazi na ukubwa wa shirika.[1][2]

Katibu kama wadhifa

hariri

Katibu wa Wizara

hariri

Katibu wa Wizara (kwa Kiingereza: Cabinet Secretary) ni neno ambalo hutumika kurejelea mtu mwenye wadhifa sawa na waziri katika nchi ya Kenya. Chini yake, kuna viongozi wa idara za wizara ambao huitwa Katibu Mkuu (kwa Kiingereza: Principal Secretary).

Katibu Mkuu

hariri

Katibu Mkuu ni cheo cha kiongozi wa baadhi ya vyama vya wafanyakazi, vyama vya kisiasa na mashirika ya kitaifa. Kwa mfano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Tanbihi

hariri
  1. "Secretary Job Information | National Careers Service". Nationalcareersservice.direct.gov.uk. 27 Januari 2012. Ilipatikana 21-03-2018.
  2. "Secretaries and Administrative Assistants : Occupational Outlook Handbook : U.S. Bureau of Labor Statistics". Bls.gov. 29 Machi 2012. Retrieved 21-03-2018.