Kawhi Leonard

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani

Kawhi Leonard (alizaliwa 29 Juni 1991) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea Marekani anayeichezea timu ya Los Angeles Clippers katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu (NBA).

Kawhi Leonard akiwa anachezea timu ya kikapu ya Toronto Raptors mwaka 2019

Kawhi alicheza misimu miwili ya mashindano ya kikapu akiwa chuoni na chuo cha San Diego State Aztecs. Mwaka 2011, Kawhi alichaguliwa kama chaguo namba 15 katika machaguzi ya wachezaji wa wadogo katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA) nchini Marekani katika timu ya Indiana Pacers. Usiku wa machaguzi hayo, Kawhi aliuzwa kwenda timu ya San Antonio Spurs.

Kawhi alifanikiwa kushinda mara moja na timu ya San Antonio Spurs tuzo ya timu bora ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA) mawaka 2014 ambapo aliweza kupewa tuzo ya mchezaji bora katika mechi ya fainali. Baadae baada ya kucheza misimu saba na San Antonio Spurs, aliuzwa kwenye timu ya Toronto Raptors mwaka 2018. Mnamo mwaka 2019, aliweza kuiongoza timu yake kupata tuzo ya timu bora ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA) na kwa mara ya pili tena aliweza kujishindia kupewa tuzo ya mchezaji bora katika mechi ya fainali.

Amefanikiwa kuteuliwa katika timu ya mastaa marekani kwa mara tatu. Mwaka 2015 na 2016, alishinda tuzo ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA) kama mchezaji mkabaji bora wa mwaka.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kawhi Leonard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.