Kelvin Pius John (wengine humuita Mbappe; alizaliwa Morogoro, 10 Juni 2003) ni mchezaji wa soka wa Timu ya taifa ya Tanzania. Ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi ambaye anacheza katika timu hiyo.

Kwa sasa yupo kwenye kituo cha michezo cha Brooke House Fooball Academy kilichopo Leicestershire nchini Uingereza.

Maisha

hariri

Wazazi wake ni wazaliwa wa kijiji cha Milama, ila mama yake alifariki Kelvin akiwa bado hata hajaonekana kimpira. Mama yake alikuwa anaitwa Halima Bakari na baba yake anaitwa Pius John, wazaliwa hawa wa Milama walienda kuishi Morogoro mjini na kuanza maisha, ndipo wakabahatika kumpata Kelvin. Baadaye kidogo mama yake akarudi Milama, baada ya kuanza kuumwa mpaka alipofariki.

Kelvin hata likizo zake huwa anakwenda Milama na kijiji kizima wanamuombea afike mbali kwani ndiye mchezaji wa kwanza kijijini na amekuwa kichocheo kikubwa kwa watoto wengi wa Milama.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kelvin Pius John kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.