Kenny Thomas (alizaliwa Islington, London, 12 Septemba 1968) ni mwimbaji kutoka Uingereza ambaye alikuwa na kazi nzuri katika miaka ya 1990, akiingiza nyimbo nane kwenye chati za UK top 40.[1][2]

Kenny Thomas
Jina Kamili Kenny Thomas
Jina la kisanii Kenny Thomas
Nchi Uingereza
Alizaliwa 12 Septemba 1968
Aina ya muziki Soul, R&B
Kazi yake Mwanamuziki
Miaka ya kazi 1988 - hadi leo

Maisha binafsi

hariri

Thomas alikulia Hillside Estate, Stamford Hill na alihudhuria shule ya Kardinali Pole Roman Catholic huko Hackney. Aliwahi kuwa bondia na fundi kwenye kampuni ya BT technician kabla ya kuanza kazi kama mwimbaji.

Sasa anaishi Costessey karibu na Norwich.[3]

Mafanikio ya Thomas yalikuja mnamo 1991 alipotoa wimbo wa kwanza Outstanding, ambao ulifika mpaka namba 12 kwenye UK Singles Chart; wimbo ambao toleo la kwanza ulitolewa na Gap Band.

Mwaka huo huo alifanikiwa kuingiza nyimbo nyingine tatu kwenye chati za UK ikiwemo uliyovuma zaidi Thinking About Your Love ambao ulifika namba 4 kwenye chati hizo na kukaa kwa wiki 13 na wimbo wa Best of You ambao ulifika namba 11 naulidumu kwenye chati kwa wiki saba.

Albamu ya kwanza ya Thomas Voices (1991) ilifikia nambari tatu kwenye chati ya albamu za Uingereza, ikiuza zaidi ya nakala 300,000.

Mnamo 1992 Thomas aliteuliwa kwenye tuzo za kila mwaka za BRIT Awards katika kategoria mbili, mwimbaji bora wa kiume wa Uingereza na mwimbaji chipukizi wa Uingereza.

Marejeo

hariri
  1. "Gig review: Kenny Thomas at O2 Academy Sheffield". Yorkshire Post (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-04.
  2. https://www.crossrhythms.co.uk/articles/music/Kenny_Thomas_Soul_Singer_In_A_Crazy_World/23202/p1/
  3. "1990s hitmaker on the road again after Covid battle". Evening News24 (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-15.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenny Thomas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.