Kentavious Caldwell-Pope

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani

Kentavious Tannell Caldwell-Pope (/kɛnˈteɪviəs/; amezaliwa Februari 18, 1993) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Marekani anaecheza timu ya mpira wa kikapu iitwayo Denver Nuggets ya Chama cha mpira wa kikapu cha Marekani (NBA). Alitajwa kuwa McDonald's All-American kama mmoja wa wachezaji bora wa mpira wa kikapu wa shule za sekondari katika darasa la mwaka 2011. Alicheza mpira wa kikapu wa ligi ya vyuo vikuu vya Marekani kwa miaka miwili akiwa na timu ya Georgia Bulldogs katika ukanda wa Kusini Mashariki Southeastern Conference (SEC), na alichaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka wa ukanda wa Kusini Mashariki akiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili mnamo mwaka 2013.[1]

Caldwell-Pope akiwa na timu ya Washington Wizards mnamo mwaka 2022

Marejeo hariri

  1. "Georgia sophomore star entering NBA draft". USA TODAY (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-06-16.