Kenya National Bureau of Statistics
Kenya National Bureau of Statistics (kifupi: KNBS; Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya) ni taasisi ya serikali ya Kenya iliyopewa kazi ya kutunza takwimu za nchi hii
Sheria ya Takwimu (Statistics Act 2006) inataja wajibu wake kama ifuatavyo:
- kuwa taasisi kuu ya serikali inayokusanya data, kuzitathmini na kusambaza taarifa zake
- kutunza data rasmi
- kuendesha sensa ya kitaifa kila baada ya miaka 10
- kujenga na kutunza mkusanyiko wa data za jamii na uchumi
- kufuata mbinu sanifu katika ukusanyaji na usambazaji wa data
- kupanga, kuruhusu na kusimamia miradi yote ya takwimu ndani ya mfumo wa takwimu wa taifa
KNBS ilitanguliwa na idara ya takwimu ya serikali. Sheria ya 2206 iliunda taasisi mpya yenye kiwango kikubwa cha madaraka ya kuendesha mambo yake bila kutegemea maagizo ya mara kwa mara kutoka serikalini.
Viungo vya Nje
hariri- Historia ya KNBS Ilihifadhiwa 8 Januari 2019 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti rasmi ya KNBS Ilihifadhiwa 29 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |