Kerron Stewart (alizaliwa 16 Aprili 1984) ni mwanariadha wa Jamaika ambaye ni mtaalamu wa mbio za 100m na 200m. Yeye ndiye aliyekuwa bingwa wa Jamaika wa mbio ya 100m katika mwaka wa 2008 akiwa na muda wa 10.80s. Alimshinda bingwa wa dunia Veronica Campbell-Brown mwaka huo na akashinda medali ya fedha katika michezo ya Olimpiki ya 2008 alipomaliza katika nafasi yapili wakiwa pamoja na Sherone Simpson katika muda wa 10.98s. Alishinda ,pia, medali ya shaba katika mbio ya 200m katika Olimpiki hiyo ya 2008 akimaliza na muda wa 22.00s. Alizaliwa mjini Kingston,Jamaika.

Mwanariadha wa Jamaika
Michezo ya Olimpiki
Medali ya fedha - 2008 - Beijing - 100 m
Medali ya shaba - 2008 - Beijing - 200 m
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia
Medali ya dhahabu - 2009 - Berlin - 4x100 m
Medali ya fedha - 2007 - Osaka - 4x100 m
Medali ya dhahabu - 2009 - Berlin - 100 m

Wasifu

hariri

Olimpiki ya 2008,Beijing

hariri
 
Kerron Stewart(katikati) na wenzake wa Jamaika baada ya kushinda katika mbio ya Olimpiki ya 2008,Beijing,Uchina

Katika Olimpiki hii alishiriki katika mbio ya mita 100. Katika mbio za kuhitimu, alichukua nafasi ya kwanza akiwashinda Ezinne Okparaebo na LaVerne Jones-Ferrette katika muda wa sekunde 11.28 na kuhitimu kushindana katika raundi ya pili. Hapo aliboresha muda wake kuwa 10.98 kushinda mbio hiyo akiwashinda Lauryn Williams na Kim Gevaert. Alishinda nusu fainali kwa muda wa 11.05 na kuhitmu nafasi ya kushindana katika fainali ya mbio hiyo. Katika mbio ya ajabu ambayo Mjamaika mwenzake,Shelly-Ann Fraser,alishinda medali ya dhahabu,Stewart na Sherone Simpson walipata medali ya fedha kila mmoja kwa muda wa 10.98s katika mbio yenye medali zote zilishindwa na Wajamaika. Wakiwa pamoja na Fraser, Simpson, Sheri-Ann Brooks, Aleen Bailey na Veronica Campbell-Brown alishiriki katika mbio ya 4 x 100m. Katika raundi ya kwanza(bila Simpson na Stewart) walichukua nafasi ya kwanza mbele ya Urusi,Ujerumani na Uchina. Muda wa Jamaika ulikuwa sekunde 42.24 na huo ndio uliokuwa muda kasi kabisa kati ya mataifa 16 yaliyoshiriki katika mbio hiyo. Kutokana na matokeo haya wao,walihitimu kushindana katika fainali ambapo wakabadilisha Brooks na Bailey kwa Simpson na Stewart. Hatimaye,hawakumaliza mbio hiyo kutokana na makosa katika kubadilishana kile kijiti kati ya wanariadha. [13]

Mbio ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha 2009

hariri

Stewart alichukua nafasi ya pili katika mbio ya 100m katika mashindano ya kitaifa ya 2009,akimaliza mbio hiyo na muda wa 10.93s na akahitimu kuingia Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009. kuja pili ya 100 m kwenye michuano 2009 Jamaika kitaifa, kumaliza katika 10.93 s na zinazotozwa kwa Mabingwa wa Dunia 2009.

Katika mbio ya 2009 ya IAAF Golden Gala,Stewart alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya 100m akimshinda bingwa wa Olimpiki,Shelly-Ann Fraser.Alishinda kwa muda wa 10.75s iliyokuwa sawa na rekodi ya mbio hiyo katika shindano hilo. Huu ndio uliokuwa muda wa kasi kabisa kuhitimiwa na mwanamke katika tukio hilo kwa miaka kumi,muda wa kasi wa tatu wa Kijamaika ikiwa nyuma ya 10.74s ya Merlene Ottey na 10.73 ya Shelly-Ann Fraser. [14]

Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009,Kerron Stewart alishinda medali ya fedha katika mbio ya 100m akiwa nyuma ya mwenzake Shelly-Ann Fraser kwa muda mdogo tu akitosheleza rekodi yake ya kibinafsi ya 10.75s.Walishinda mbo hiyo Wajamaika wawili katika nafasi ya kwanza na ya pili. Stewart hakushiriki katika mbio ya 200m kwa sababu ya jeraha kwenye kifudio lakini akashiriki katika mbio ya 4 x 100m ambayo walishinda medali ya dhahabu.

Mafanikio

hariri
Mwaka Mashindano Pahali pa kushindana Matokeo Aina ya Mbio
2000 Mashindano ya Mabingwa Vijana wa Dunia ya 2000 Santiago, Chile 2 4 x 100 m
2001 Mashindano ya Mabingwa Vijana wa Dunia katika Riadha ya 2001 Debrecen, Hungaria 2 100 m
2 Mbio ya kubadilishana
2002 Mashindano ya Mabingwa Vijana wa Dunia ya 2002 Kingston, Jamaica 4 100 m
1 4 x 100 m
2007 Mashindano ya Mabingwa katika Riadha ya 2007 Osaka, Ujapani 7 100 m
2 4 x 100 m
2008 Olimpiki ya 2008 Beijing, Uchina 2 100 m
3 200 m
2009 Mashindano ya Mabingwa katika Riadha ya 2009 Berlin, Ujerumani 2 100m

Muda bora za kibinafsi

hariri
  • Mbio ya mita 100 - 10.75 s (2009)
  • Mbio ya mita 200 - 21.99 s (2008)

Marejeo

hariri
  1. a b c Athlete biography: Kerron Stewart, beijing2008.cn,
  2. ^ Foster, Anthony (2009-06-28). Bolt 9.86 and Fraser 10.88; Walker and Phillips excel over hurdles - JAM Champs , . IAAF.

Viungo vya nje

hariri