Sherone Simpson
Sherone Simpson (alizaliwa 12 Agosti 1984) ni mwanariadha wa nchi ya Jamaika ambaye huiwakilisha nchi yake katika mashindano ya kimataifa. Alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya 4 x 100m katika mashindano ya Olimpiki ya 2004 na medali ya fedha katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2005.Alishinda medali ya fedha katika mbio ya 100m katika Olimpiki ya 2008 baada ya kukimbia kwa muda mmoja na mwenzake wa Jamaika ,Kerron Stewart. Muda wake wa kibinafsi wa 10.82 s katika mbio ya 100m,Simpson ndiye mwanariadha mwanamke wa nne bora nchini Jamaika.Mbele yake ni Merlene Ottey,Shelly-Ann Fraser na Kerron Stewart. Muda wake bora wa 22.00 s katika mbio ya 200m ndio muda wa nne bora katika orodha ya Jamaika akiwa nyuma ya Merlene Ottey,Grace Jacson,Juliet Cuthbert,Veronica Campbell-Brown na Kerron Stewart. Amekimbia mbio ya 200m na muda huu mara mbili. Kocha wa Simpson ni Stephen Francis mjini Kingston.Jamaika, anaposoma katika Chuo Kikuu cha Teknolojia. Yeye ,pia, alisoma katika shule ya Manchester High.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Riadha ya Wanawake | ||
Anawakilisha nchi :Jamaika | ||
Michezo ya Olimpiki | ||
Dhahabu | 2004 Athens | 4 x 100 |
Fedha | 2008 Beijing | 100m |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF katika Riadha | ||
Fedha | 2005 Helsinki | 4x100 m |
Michezo ya Jumuia ya Madola | ||
Dhahabu | 2006 Melbourne | 200 m |
Dhahabu | 2006 Melbourne | 4 x 100 m |
Wasifu
haririSimpson alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya wanawake ya 200 m katika Michezo ya Jumuia ya Madola ya 2006 , huku akishinda Veronica Campbell.Katika mbio hizo, Jamaika ilishinda medali za dhahabu kwa mbio za 100m na 200m. Jamaika ilishinda ,pia, medali zote za dhahabu katika mbio za kuruka viunzi.
Katika Olimpiki ya 2008 mjini Beijing alishiriki katika mbio ya 100m. Katika mbio za mchujo,alikuwa wa tatu nyuma Yevgeniya Polyakova na Jade Bailey katika muda wa 11.48s na kuhitimu awamu ya pili. Katika awamu ya pili aliboresha muda wake ukawa 11.02s na kushinda mbele ya Muna Lee na Chandra Sturrup. Katika mbio za nusu fainali alikuwa nambari ya nne na 11.11 s akapata nafsi katika fainali. Katika mbio za ajabu na wenzake wa Jamaika,Shelly-Ann Fraser na Kerron Stewart, walishinda medali huku Fraser akipata ya dhahabu na Stewart & Simpson wakipata ya fedha. Akiwa pamoja na Fraser,Stewart, Sheri-Ann Brooks,Aleen Bailey na Veronica Campbell-Brown alishiriki katika mbio ya 4 x 100. Katika mbio za mchujo(bila Simpson na Stewart) walikuwa wa kwanza mbele ya Urusi,Ujerumani na Uchina. Muda wa sekunde 42.24 ndio uliokuwa bora kabisa kati ya mataifa 16. Kutokana na matokeo haya, walihitimu kushiriki katika mbio ya fainali.Katika fainali waliweka Simpson na Stewart badala ya Bailey na Brooks. Hatimaye,hawakumaliza mbio yao kutokana na makosa katika kubadilishana kijiti cha kumpa mwanariadha mwenzako. [14]
Ubora wa binafsi
haririShindano | Muda | Upepo | Pahali | Tarehe |
---|---|---|---|---|
100 m | 10.82 | -0.7 | Kingston, Jamaika | 24 Juni 2006 |
200 m | 22.00 | -0.3 | Stockholm, Uswidi | 25 Julai 2006 |
+1.3 | Kingston, Jamaika | 25 Juni 2006 | ||
400 m | 51.25 | Kingston, Jamaika | 22 Machi 2008 |
Marejeo
hariri- Athlete biography: Sherone Simpson, beijing2008.cn,
Viungo vya nje
hariri- IAAF profile for Sherone Simpson
- Picha za Sherone Simpson
Alitanguliwa na Allyson Felix |
Wanawake Bora wa Mwaka katika mbio ya 200m 2005 |
Akafuatiwa na Allyson Felix |