Kifupi

(Elekezwa kutoka Kifupisho)

Kifupi au kifupisho ni njia ya kutaja au kuandika neno kwa namna fupi kuliko kawaida.

Watu hutumia kifupi mara nyingi wakiandika neno au kundi la maneno fulani mara nyingi. Hasa pale ambapo nafasi ya kuandika ni ndogo vifupisho vya aina hii ni vya kawaida kama vile kwenye SMS, kamusi au orodha za vitu.

Vifupisho vimekuwa pia kawaida kutaja vitengo vya serikali kama "JKT" (jeshi la kujenga taifa), kampuni kama "SMP" (Southern Paper Mills) au vyama vya kisiasa kama "CCM" (Chama cha Mapinduzi).

Vifupisho vya pekee huitwa pia akronimi: ni maneno ambayo yameunganishwa kwa herufi za kwanza za maneno mengine. Mifano yake ni UKIMWI (=Uhaba wa KInga MWIlini) au Laser (= Laser - Light Amplification through Stimulated Electron Radiation).

Vifupisho vinatumiwa mara nyingi kwa kubadilisha maana asilia kwa kusudi la kutania au kufanya jambo linalojadiliwa kuonekana kama kichekesho.

Mifano yake ni tafsiri ya FFU (kikosi cha polisi ya Tanzania cha kukandamiza ghasia) kama "Fanya Fujo Uone" au ya CCM (chama tawala cha miaka mingi nchini Tanzania) kama "Chukua Chako Mapema".

Vifupi katika kamusi

hariri

Kamusi ya KKS inatumia vifupi vifuatavyo:

  • agh. - aghlabu
  • ele - elekezi
  • fiz - fizikia
  • kb - kibaharia
  • kd - kidini
  • kem - kemia
  • kh - kihusishi
  • ki - kiingizi
  • kl - kielezi
  • k.m. - kwa mfano
  • kt - kitenzi
  • ku - kiunganishi
  • k.v. - kama vile
  • ksh - kishairi
  • kv - kivumishi
  • kw - kiwakilishi
  • kz - kizamani
  • ms - msemo
  • mt - methali
  • nh - nahau
  • n.k. - na kadhalika
  • nm - nomino
  • sie - sielekezi
  • taz. - tazama

Vifupi vya kisiasa na vya kiserikali

hariri

Viungo vya nje

hariri
  • Acronym Finder - largest acronym site with many ways to search for acronyms and abbreviations in many languages. Over 10 year history.
  • All Acronyms - a website with a large number of abbreviations and acronyms