Kihonda maghorofani
Kihonda Maghorofani ni mtaa wa kata ya Kihonda inayopatikana katika wilaya ya Morogoro mjini, katika mkoa wa Morogoro.
Kata hiyo ina shule nyingi sana.
Kata ya Kihonda ilikuwa ikisumbuliwa na uhalifu, kama vile ujambazi na wizi. Hapo wanakata wakaitisha kikao ili kuzuia uhalifu huo wakapata njia ya kwamba usiku kuwe na walinzi waitwao sungusungu. Hao walilinda kwa muda wa wiki moja na kumkamata mwizi mmoja ambaye alipelekwa mahakamani akafungwa kifungo cha miaka miwili. Alipotoka mahakamani aliacha wizi. Ingawa walikamatwa wezi, ulinzi uliendelea mpaka wezi walipotokomea na kwa sasa katika kata ya Kihonda Maghorofani hakuna uhalifu tena.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|