Kiini cha seli (kwa Kiingereza cell nucleus) ni sehemu ndogo ndani ya seli ya kiumbehai wa aina ya eukaryota inayobeba habari za jenetikia, yaani urithi wa tabia za kiumbehai. Ndani ya kiini kuna nyuzi za kromosomu zenye DNA. Hizi zinapatikana kama mkusanyiko wa nyuzi (nucleolus ~ ka-kiini) ndani ya kiini.

Kiini cha seli
Maelezo ya majina ya Kiingereza tazama chini katika matini
Seli zilizotiwa rangi ya kuonyesha DNA ndani ya viini; seli upande wa kushoto inaandaa kujigawa na hapa DNA ndani yake imeshajikaza, tayari kwa ugawaji

Mwili wa binadamu huwa na seli milioni kadhaa, na nyingi zina viini vya seli. Mfano wa seli ya binadamu isiyo na kiini ni seli nyekundu za damu.

Kiini chenyewe ndani ya seli hukingwa kwa utando wa kiini cha seli (ing. nuclear envelope au nuclear membrane). Utando huu unazuia molekuli kubwa lakini inaruhusu kupita kwa proteini maalumu kwenye nafasi maalum (nuclear pores).

Seli za mwili zinajigawa muda wote. Wakati wa kujigawa, kromosomu zinajikaza kwa pande mbili halafu kiini kinavunjika; utando wa kiini unayeyushwa, na seli mbili mpya zinatokea. Ndani ya seli mpya kiini kinaundwa upya kwa kutengeeza utando wa kiini mpya.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiini cha seli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.