Eukaryota
Eukaryota ni kundi kubwa la viumbehai ambavyo vina seli zenye kiini cha seli na utando wa seli. Mimea, wanyama na fungi wote tunaoona huhesabiwa humo.
Zinahesabiwa kwa jumla kama domeni kati ya viumbehai na domeni nyingine ni bakteria na archaea ambavyo ni viumbe vidogo sana vinavyoonekana kwa hadubini tu.
Eukaryota walio wengi wana seli nyingi lakini hasa protisti na sehemu za fungi zina seli moja tu.
Mfumo wa seli
haririSeli za eukaryota ni kubwa kuliko seli za bakteria na archaea. Ndani ya seli zao kuna oganeli ambazo ni kama viungo vya mwili lakini vina shughuli maalumu ndani ya seli.
Oganeli inayojulikana zaidi ni kiini cha seli inayotunza sehemu kubwa ya DNA yake.
Seli za eukaryota huwa pia na kitu kinachofanana na kiunzi cha mifupa kwenye mwili kinachojengwa kwa vimirija vya protini za pekee ambazo ni gumu kiasi kuliko ektoplasma inayojaza seli.
Kimsingi seli za eukaryota huwa na
- kiini cha seli,
- utando wa seli (ganda la nje pamoja na maganda ya ndani) na
- utegili (ektoplasma) unaojaza chumba ndani ya utando. Ndani ya utegili kuna sehemu nyingine zenye kazi mbalimbali kama ribosomu au dutuvuo (mitokondria).
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eukaryota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |